
Mchezaji
wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima akichuana na beki wa timu ya Mtibwa
Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa
Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, Mpira umekwisha na Yanga
imefanikiwa kuitandika Mtibwa Sugar Magoli 3-01 bila huruma katika
kipindi cha pili cha mchezo huo.
Magoli ya Yanga yamefungwa na wachezaji Keneth Asamoah,Shamte Ally,
Khamis Kiiza , na kwa upane wa timu ya Mtibwa Sugar mfungaji alikuwa
Issa Rashid aliyeipatia timu hiyo goli la kufutia machozi.

Refarii
wa mchezo huo akinyoosha mkono wake juu kuashiria timu ya Yanga ipige
mpira wa adhabu kuelekea lango la timu ya Mtibwa Sugar.
Mmoja wa Mashabiki wa timu ya Yanga akiwa amejipaka masizi usoni mwake ikiwa ni moja ya staili ya ushangiliaji kwa timu yake.
No comments:
Post a Comment