Andre
Villas-Boas alikutana kwa siri mjini London na mkurugenzi wa AS Roma
Franco Baldini mwezi uliopita kuzungumza juu ya mreno huyo kuwa kocha wa
klabu hiyo msimu ujao imefahamika.
AVB,
ambaye alitimuliwa na Chelsea juzi Jumapili, amekuwa akiwindwa na seria
A club kumbadili kocha wa sasa Luis Enrique kipindi kijacho cha
kiangazi.
Mtandao
wa Goal.com umeweka wazi kwamba mazungumzo katika ya AVB na Baldini
yalifanyika katika mgahawa ambao upo karibu na makazi ya Baldini, ambaye
aliacha kazi katika timu ya taifa ya England na kujiunga na Roma in
October.
Villas-Boas
aliulizwa na Baldini kama angekuwa interested kumrithi Enrique, ambaye
inasemekana ndio kocha Anayetajwa kumrithi Pep Guardiola akiwa aamua
kuhama kocha ataamua kuondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu.
Mreno
inasemekana alimjibu msaidizi wa zamani wa Capello kwamba alikuwa
akihofia kufukuzwa kazi wakati wowote kutokana na mfululizo wa matokeo
mabaya, hivyo alikuwa tayari kuhamia Roma.
Pia Goal.com imefichua kwamba AVB alishakutana na watu wa
AS Roma kabla ya Enrique hajahamia klabuni pale wakati alipokuwa Porto
lakini watoto wa PAPA walishindwa dau la kumtoa Porto paundi
millioni13.4 ambayo ilikuja kulipwa na Chelsea.
Enrique
anaonekana sio mtu wa kufukuzwa Roma – ambayo ni yasita katika msimamo ,
lakini kuna vishiaria vyote vinavyoonesha kwamba hatakuwepo Italy msimu
ujao.
Chanzo
cha habari kutoka kwa Mhispania huyo kinasema kuna makubaliano yam domo
kati ya raisi wa Barcelona Sandro Rossell kuchukua nafasi ya Pep ikiwa
kocha huyo wa sasa ataamua kuachana na klabu hiyo kwa sasa.
Akiongea baada ya kufungwa katika derby dhidi ya Lazio wikiendi iliyopita, Enrique alisema: “ Kama mpaka sasa siaminiki kama kocha sahihi wa Roma then nitaondoka bila matatizo yoyoteKwa hisani ya shafih dauda
No comments:
Post a Comment