Marehemu Steven Kanumba na Baba yake Charles Kaumba
---
Baba mzazi wa Kanumba anaeishi Shinyanga amefunguka na , kuzungumza Exclusive na millardayo.com
na kusema kwamba sasa yuko tayari kuja Dar es salaam kushughulikia
swala la Mirathi baada ya kudai kwamba mama mzazi wa Kanumba ambae yuko
Dar ameanza kuharibu issue ya mirathi.
Amesema
“Tutakaa kikao Jumamosi kuteua msimamizi wa mirathi, mama ameteua
kinyemela bila kunishirikisha, hilo swala nimelipinga nimewasiliana nae
kumuuliza kwa nini kafanya hivyo akawa ana jiuma uma tu, kwa nini
umeokota watoto kuwadanganya danganya kikao cha kusimamia mirathi si
tungekaa pamoja? akachukua watoto wangu wako huko wasichana wawili
lakini walipotoka kikaoni wakanipigia simu kwa sababu hawakuridhika.”
Baba
huyu mzazi wa Kanumba amezidi kufunguka kwamba “mama hakusema lolote
baada ya mimi kumwambia huo mkutano ni batili lakini akauliza kwani yeye
akiteuliwa peke yake kuna ubaya gani, nikamwambia ingekua halali
kuteuliwa peke yako kama tungekua tunaishi pamoja lakini tulishatengana
kwa hiyo pande zote mbili ni lazima ziteue, huyu mama aliwateua hao
watoto wangu wawili alafu akamchukua kinyemela na kumlipia nauli kijana
wangu mwingine anaitwa Ayubu ambae ni mtoto wa dada yangu.”
“Tulikubaliana
kwamba mpaka tufanye siku 40 za marehemu sasa yeye kaanza kukaa
kinyemela tena, maajabu maajabu.. sasa hivi tunakaa huku huku kikao cha
wa wanandugu cha mzee Kanumba wanatoka Sengerema Mwanza na Bariadi
Shinyanga, kama wakiniteua kwenda Dar es salaam nitakwenda.”
Source: Millardayo.com
No comments:
Post a Comment