Aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (katikati), akiwa amekaa
na Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari
(kushoto), akimpa moyo, baada ya hukumu kutolewa.
Mmoja
wa wafuasi wa Chadema, Naomi Solomon (56), akiwa amepoteza fahamu, mara
baada ya mahakama kutangaza kumtengua Ubunge Godbless Lema.
Makada watatu waliofungua kesi dhidi ya Lema, Agnes Mollel…
Mmoja
wa wafuasi wa Chadema, Naomi Solomon (56), akiwa amepoteza fahamu, mara
baada ya mahakama kutangaza kumtengua Ubunge Godbless Lema.
Makada
watatu waliofungua kesi dhidi ya Lema, Agnes Mollel (kulia), Happy
Kivuyo (mwenye koti jekundu) na mwisho Musa Mkanga, wakifurahi
mahakamani mara baada ya hukumu kutolewa.
Aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katikati
akihutubia umati wa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika
mahakamani kusikiliza shauri la kupinga ubunge wake, ambapo mahakama
imeutengua ikidai Lema alikiuka sheria za uchaguzi na kuamuru uchaguzi
urudiwe.
Askari
polisi wakiwa eneo la mahakama wakiimarisha ulinzi muda mfupi baada ya
mahakama kutengua ubunge wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutoka
Chadema.
Lema
akiwatia moyo wafuasi wa chadema katika eneo la mahakama baada ya
kupokea matokeo ya kutengua ubunge wake leo, huku akieleza kuwa hata
kata rufaa ila anasubiri tume ya uchaguzi itangaze rasmi kuanza kwa
uchaguzi katika jimbo la Arusha Mjini.
Polisi wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Umati
wa wafuasi wa Chadema ukisikitishwa na uamuzi wa mahakama ya mjini
Arusha, ulitolewa na Jaji, Gabriel Rwakibarila wa mahakama kuu kanda ya
Sumbawanga.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment