marehemu enzi za uhai wake
Enzi za uhai wake Marehemu
Mwenyekiti
wa Chadema, Kata ya Usa River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha,
Msafiri Mbwambo, (32) mkazi wa Lake Tatu, ameuawa kinyama kwa kuchinjwa
shingoni kuanzia upande wa nyuma lakini wakiacha koromeo na mwili wake
kutelekezwa makaburini.
Tukio
hilo lililitokea majira ya saa 3:00 usiku eneo la Mukidoma, huko Usa
River, ambapo wauaji hao wasiofahamika wanadaiwa kuwa walitumia panga
kumchinja na kisha kutokomea.
Haijafahamika
iwapo tukio hilo ni kisiasa au la lakini Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Arusha, Thobias Andengenye, alitibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
Katibu
wa Chadema wa Wilaya ya Arumeru, Totinan Ndonde, alisema jana jioni
kwa njia ya simu kuwa hawezi kuhusianisha mauaji hao kwa asilimia 100
kuwa ni ya kisiasa. Hata hivyo, alisema wakiangalia historia ya kampeni
za uchaguzi mdogo kuanzia Igunga na huo wa hapo uliofanyika hivi
karibuni hapo Arumeru, kuna uwezekano wa kuhusisha mauaji hayo na
masuala ya siasa. Hakufafanua zaidi.
Chanzo
kingine cha habari kimedai kuwa kulikuwa na ugomvi wa ubadhirifu wa
mradi wa maji ambapo marehemu aliahidi kuwataja waliokula fedha hizo.
“Inawezekana
wauaji wameamua kumuondoa duniani kwa hofu ya kutajwa kwenye
ubadhirifu huo,” kilisema chanzo hicho. Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla
ya tukio hilo marehemu Mbwambo alikuwa na wenzake kwenye eneo la
sterehe huku yeye akiwa hanywi chochote, lakini ghafla alipigiwa simu na
watu hao, wakidai kuwa kulikuwa na wanachama wa chama kimoja cha siasa
wanataka kurudisha kadi zao cha chama na kujiunga na Chadema.
Habari
zilisema kuwa marehemu Mbwambo, alichukua pikipiki na kuwafuata watu
hao, lakini, hata hivyo, hakurudi hadi mwili wake ulipokutwa
umetelekezwa kandokando ya barabara eneo la makaburi, huku pikipiki na
vitu vingine alivyokuwa navyo vikiwa vimebaki eneo hilo bila
kuchukuliwa na wauaji hao.
Hata
hivyo, chanzo cha tukio hilo hakijajulikana ila taarifa za awali
zinahusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa kwani kabla ya hapo baada
ya uchaguzi kumalizika katika Jimbo la Arumeru Mashariki malumbano ya
masuala ya kisiasa na kukamiana yalikuwa bado yakiendelea eneo hilo.
Kamanda
Andengenye alisema polisi bado wanafanya uchunguzi kuhusiana na tukio
na kwamba hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Alisema mwili wa merehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.
Hili
ni tukio la pili la mauaji ya kutisha yaliyoliyotokea wilayani humo
hivi karibuni, ambapo tukio wiki iliyopita watu wanne walikutwa
wamekufanya kwa kunyongwa na maiti zao kutupwa eneo la Chekereni,
wilayani humo.
sijui kama ni mungu kweli huw aanapang ahaya mambo ila apumzike kwa amani kamanda!
ReplyDelete