Mshitakiwa
Juliana Ibrahimu akitolewa nje ya chumba cha mahakama kuu baada ya
kuzirai kutokana na kuhukumiwa kutumikia jela miaka mitatu baada ya
kukiri kosa la kuuwa bila kukusudia.
Askari
polisi wa kike wakimpunguzia nguo mshitakiwa Juliana Ibrahimu ili
waweze kupepea upepo aweze kuzinduka baada ya kuzirai kutokana na
kuhukumiwa adhabu ya kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kuuwa jirani
yake Maria Musa, bila kukusudia.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Mwanamke
mkazi wa kijiji cha Musimihi tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida,
Juliana Ibrahimu (52),ameanguka kizimbani na kisha kuzirai na kupoteza
fahamu, baada ya kuhukumiwa na mahakama kuu kanda ya Dodoma, kutumikia
jela miaka mitatu.
Mahakama
kuu kanda ya Dodoma inayoendelea na vikao vyake mjini hapa, ilimhukumu
Juliana hukumu hiyo,baada ya kukiri kosa la kumuua jirani yake, Maria
Musa, bila kukusudia kwa madai ya kunyimwa makande kwenye sherehe ya
harusi.
Mshitakiwa
Juliana, alihukumiwa adhabu hiyo pamoja na mtoto wake Pendo Yohana,
ambaye naye atatumikia jela miaka mitatu kwa kukiri kosa hilo.
Baada
ya washitakiwa hao kusomewa shitaka hilo la mauaji ambalo walilitenda
agosti tano mwaka 2006, wote kwa pamoja, bila hofu kila moja kwa wakati
wake alikiri kosa hilo .
Awali
mwanasheria wa serikali Ahmed Seif, alidai mbele ya mrajisi wa mahakama
hiyo, Renatus Rutatinisibwa, kuwa mnamo agosti tano mwaka 2006, muda
usiofahamika,washitakiwa wote kwa pamoja, walimpiga Maria na kusababisha
kifo chake siku 27 baadaye.
Alisema
siku ya tukio, mshitakiwa Juliana akiwa amefuatana na mtoto wake Pendo,
walikwenda nyumbani kwa marehemu (Maria) kumuliza ni kwa nini
aliwanyima makande kwenye sherehe ya harusi (harusi hiyo iifanyika
4/8/2006).
Seif alisema marehemu aliwajibu kuwa hawezi kujibu swali hilo na kwamba mwenye uwezo wa kulijibu swali hilo , ni Dilu Mohammed.
Alisema washitakiwa walikasirishwa na jibu hilo liliyotolewa na marehemu na ndipo walipoanza kumshambulia.
Baada
ya kutolewa kwa uhukumu hiyo, mshitakiwa wa kwanza,Juliana akiwa bado
yupo kizimbani, alidondoka chini na mrajisi Rutatinisibwa, akaamuru
atolewe nje kwenda kupepewa upepo.
Kwa hisani ya Mo Blog
Kwa hisani ya Mo Blog
No comments:
Post a Comment