Tabia ya timu za kisudani
kuzipokea vibaya timu pinzani zinapoenda kucheza nchini kwao umeendelea,
baada ya Simba sasa ni TP Mazembe ambao jana mashabiki wa klabu ya Al
Merreikh ya Sudan wameufanyia fujo msafara wa klabu ya Tout Puissant
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Khartoum,
wakidai na wao walipokewa vibaya na klabu hiyo mjini Lubumbashi wiki
mbili zilizopita.
Mazembe yenye washambuliaji
wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ipo
Khartoum kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya Merreikh, hatua ya 16 Bora.
Katika vurugu hizo, basi
walilokuwa wamepanda wachezaji wa Mazembe limevunjwa vioo ambapo hali
za wachezaji bado hazijajulikana na sasa mechi hiyo iliyopangwa
kufanyika kwenye Uwanja wa Omdurman, hatima yake ipo mikononi mwa
Shirikisho la Soka Afrika (CAF)- ambalo linatarajiwa kuchukua hatua muda
mfupi ujao, kubwa zaidi ikitarajiwa kuifuta mashindanoni Merreikh na
kuifungia, hivyo Mazembe kusonga mbele. (kwa mujibu wa shaffihdauda.com)
Simba ambayo nayo iko Sudan
kwa ajili ya mechi yao ya jumapili nayo imekiri kufanyiwa vitimbi
ikiwemo kuzimiwa taa za uwanja wakiwa mazoezini, kulazwa hosteli badala
ya hotelini pamoja na fitina nyingine kibao.
No comments:
Post a Comment