KATIBU
mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah ametangaza
kujivua nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya
Yanga.
Osiah
amesema kuwa analazimika kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za shirikisho hilo na atawasilisha barua kwa katibu mkuu wa
Yanga, Mwesiga Selestine.
Alisema
kuwa licha ya kuteuliwa muda mrefu kushika wadhifa wa ukatibu wa TFF,
alishindwa kuwasilisha barua ya kujitoa katika kamati ya uchaguzi
kutokana na kuingwa na majukumu ndani ya shirikisho hilo.
“Nimelazimika
kufanya hivyo kwani kwa sasa Yanga inahitaji kufanya uchaguzi mdogo kwa
lengo la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi
walioachia ngazi Yanga hivyo inabidi nafasi yangu ijazwe ili kamati
iweze kuendesha mchakato wake kikamilifu,”alisema.
TFF
kupitia kamati ya uchahizi iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius
Lyato iliiagiza kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake
Jaji John Mkwawa ifanye uchaguzi wake kuziba nafasi za nane za viongozi
waliojiuzulu na mjumbe mmoja aliyefariki dunia.
Hatua
hiyo inafuati hivi karibuni kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Yanga Lloyd
Nchunga kutokana na shinikizo la baadhi ya wanachama wakiongozwa na
baraza la Wazee waliomtaka kufanya hivyo kwa madai ya kutoiletea
mafanikio klabu na hatimaye kupokwa ubingwa wao wa ligi kuu bara
ulioenda kwa Simba na wao kuishia nafasi ya tatu.
Awali
makamu mwenyekiti wa Yanga Davis Mosha alitangaza kujiengua katika
uongozi miezi michache baada ya kuchaguliwa kwa madai ya kutoelewana na
Nchunga, huku mjumbe wa kamati ya utendaji, Theonest Rutashoborwa
alifariki dunia.
Kama
hiyo haitoshi, wajumbe wengine walioachia ngazi Yanga ni pamoja na Seif
Ahmed, Mbaraka Igangula, Mzee Yusuf, Ally Mayay, Charles Mgondo na
Mohammed Bhinda.
No comments:
Post a Comment