Pages

Wednesday, May 16, 2012

EXCLUSIVE: NIZAR KHALFAN _ SIJASAINI YANGA WALA PENGINE POPOTE ACHENI KUZUSHA


Siku mbili baada ya magazeti na baadhi ya vyombo vya habari kueneza story kwamba kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar ambaye alikuwa nje akicheza Vancouver Whitecaps kabla ya kuhamia Philadephia - Nizar Khalfan kwamba amesaini miaka 2 kuichezea Yanga, leo nimeongea na Nizar mwenyewe ambaye amekana kutia saini ya aina yoyote na klabu ya jangwani.
"Kiukweli nimesikitishwa sana na hizi taarifa kwamba sijui nimesaini kuichezea Yanga kwa sababu ni mambo ambayo hayana ukweli kabisa. Mwanzoni ilisemekana nimesaini Simba lakini haikuwa ukweli, sikatai nimeshafuatwa na baadhi ya timu hapa Tanzania nijiunge nazo lakini na mimi naangalia vigezo vyangu ndipo nitakapochukua maamuzi. Lengo langu ni bado niende nikacheze nje ya nchi katika soka la kulipwa, hivyo hata kama ikitokea nimejiunga na timu yoyote ni lazima mkataba uwe wa muda mfupi ambao utakuwa na vipengele ambavyo havitakuwa na vikwazo vinavyoweza kunifanya nisitimize malengo yangu ya kwenda kucheza nje. Hali halisi kwa sasa ipo hivyo, sina timu kwa sasa hata mazoezi nafanya pale muhimbili na timu ya Binslum." - alisema Nizar Khalfan.
                                            kwa hisani ya shaffih dauda blog

No comments:

Post a Comment