Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa hospitalini nchini India.
Sajuki akiwa amepumzika, pembeni ni mkewe Wastara Juma.
Stori: Imelda Mtema
HEBU
mwacheni Mungu aitwe Mungu! Hatimaye habari njema kutoka katika
Hospitali ya Saifee iliyopo jijini Mumbai, India anakotibiwa staa wa
filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ zinatia faraja kwa
Watanzania, Ijumaa Wikienda linakupa stori ‘exclusive’ kutoka nchini
humo.
ANYANYUKA KITANDANI, AONGEA
Habari
hizo njema zinaeleza kuwa Sajuki aliyeambatana na mkewe, Wastara Juma
na kaka yake, hatimaye ameweza kunyanyuka kitandani na kuongea tofauti
na siku aliyoondoka Bongo na mwanzoni alipofikishwa hospitalini hapo.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu,
Wastara alisema Sajuki alikuwa amepata nafuu na hali siyo mbaya kwani
alikuwa na uwezo wa kuzungumza hivyo akampa simu ili azungumzie afya
yake yeye mwenyewe jinsi anavyojisikia.
SAJUKI LAIVU
Sajuki alipopewa simu alianza kwa kuwashukuru wale wote wanaomuombea dua na kujitolea kwa hali na mali ili kuokoa uhai wake.
“Namshukuru sana Mungu naendelea vizuri. Nilichukuliwa vipimo na nikabainika kuwa na uvimbe mwingi sehemu mbalimbali tumboni.
“Madaktari walibaini kuwepo kwa uchafu kwenye mapafu. Mwanzoni waligundua nina tatizo la kupumua na kukaukiwa damu.
“Wamelishughulikia
hilo kwanza na hapa nilipo nimezungukwa na madawa, kwa kweli najisikia
nafuu,” alisema Sajuki kwa sauti ya kukwaruza.
MADAKTARI
Sajuki
alisema alipokelewa vizuri lakini kabla ya kuanza matibabu ya uvimbe
tumboni, madaktari walilazimika kumtibu kwanza tatizo la damu na pumzi
hivyo matibabu ya kilichompeleka hospitalini hapo (uvimbe) yakawekwa
pembeni.
WASTARA ATIA NENO
Kwa
upande wake, Wastara alisema kuwa Sajuki alipaswa kupatiwa matibabu kwa
wiki mbili ndipo warejee nyumbani lakini kwa hali halisi inaonekana
watakaa zaidi kwani tayari wiki mbili zimekatika.
MATIBABU YAANZA
Wastara
alisema kuwa baada ya kumalizika kwa tatizo la pumzi na kupungukiwa
damu, madaktari wameanza vipimo vya tatizo la uvimbe na kusisitiza kuwa
uzi ni uleule wa kumwombea mumewe ili arejee katika siha njema.
TUMEFIKAJE HAPA?
Sajuki
alianza kusumbuliwa na uvimbe mwaka jana ulioanzia mkononi na baadaye
ndani ya mwili kwenye ini na sasa madaktari wanasema siyo kwenye ini tu
bali na sehemu nyingine tofauti za tumboni.
HABARI KWA HISANI YA GPL NA FREDY NJENJE
No comments:
Post a Comment