Pages

Wednesday, May 16, 2012

KING KENNY DALGLISH ATIMULIWA LIVERPOOL

 

Masaa machache baada ya kutoka Marekani kuzungumza na wamiliki wa klabu ya Liverpool, leo kocha King Kenny Dalglish ametimuliwa kazi ya ukocha pale Anfield.

Kenny Dalglish anaondoka Liverpool miezi 16 baada ya kuichukua timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha Roy Hodgson mwezi January 2011. Dalglish ambaye ameiongoza Liverpool kubeba kombe la Carling Cup msimu huu kabla hawajafungwa na kwenye fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea.

Lakini kushika nafasi ya nane kwenye premier league kulikuwa chini ya mategemeo ya wamiliki waliotumia kiasi kingi cha pesa wakitegemea angalau kupata nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya mabingwa ya ulaya.
                                       Habari kwa hisani ya shaffih blog

No comments:

Post a Comment