Kajala Masanja kuli, akiwa amejifunika usoni na kushoto katika pozi
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya msanii
wa filamu nchini Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo ya kutaka kesi yao ihamishiwe kwa hakimu mwingine ili iweze kuendelea kusikilizwa. Kajala
na mumewe waliwasilisha maombi hayo baada ya kupokea taarifa kuwa
hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yao Sundi Fimbo yupo likizo ya uzazi
. Maombi yao yalitupiliwa mbali na Hakimu Frank Moshi ambaye alisema amepokea jalada la kesi hiyo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi. “Nimewasiliana
na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Ilvin Mgeta , amesema kwa kawaida shauri
halifanyiwi mabadiliko iwapo hakimu yupo likizo na kwamba huo utakuwa
ni usumbufu,” alisema hakimu huyo. Baada ya uamuzi huo alipanga kesi hiyo iahirishwe hadi Juni 5, mwaka huu itakapotajwa mpaka hakimu atakapomaliza likizo yake. Kajala
Masanja na mumewe Faraja Chambo wanakabiliwa na mashtaka matatu kula
njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na kutakatisha fedha haramu.
No comments:
Post a Comment