Pages

Tuesday, May 15, 2012

MASHINE CHACHE ZA MIONZI ZACHANGIA KUSHUKA KWA HUDUMA ZA MATIBABU YA KANSA OCEAN ROAD


NA MWANDISHI WETU
 
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Saratani Ocean Road, Twalibu Ngoma amekiri kuwa kuanguka kwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo, kumechangiwa na   uwezo mdogo wa serikali wa kununua mashine za mionzi  kwa ajili ya wagonjwa hao.
 
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi huyo aliwataka watanzania kufahamu kuwa hadi sasa hospitali hiyo ina mashine moja ambayo haiendani na idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.
 
Ngoma alisema ili huduma hizo ziweze kuwa za uhakika, hospitali hiyo inapaswa kuwa na mashine nane (8), ambapo kwa sasa ipo mashine moja ambayo haikidhi.
 
“Unajua gharama za kununua mshine moja hadi kufungwa inafikia gharama ya shil. Bilioni 2, fedha ambazo kwa sasa serikali haina uwezo wa kuzipata mara moja”alisema Ngoma.
 
Ngoma alisema kutokana na uwepo wa mashine hiyo moja kumesababisha wagonjwa zaidi ya 100 hadi 200 kulazimika kupatiwa huduma hiyo ya mionzi kitendo ambacho hakilingani na matibabu hayo.
 
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna wagonjwa 40000 wanaohitaji kupatiwa matibabu lakini hata hivyo kati ya hao ni 4000 pekee ndio wanaopati huduma hiyo.
 
Aliwataka Wanzania kutambua kuwa kuanguka kwa huduma za matibabu ya saratani katika katika hospitali hiyo hakutokani na mtu bali kunasababishwa na uwezo mdogo wa kifedha wa serikali.
 
Akizungumzia matatizo ya manesi ya kutishia kuandamana kutokana na kutolipwa malipo ya saa za ziada za kazi, Mkurugenzi huyo alisema hiyo ni moja ya haki yao ya msingi ili mradi wawe na sababu za msingi.
 
Alisema kima inavyoeleweka kuwa hospitali hiyo haina kibali cha kulipa malipo ya ziada ambapo hadi sasa hakuna Nesi anayefanya baada ya masaa ya kawaida (overtime).
kwa hisani ya fullshangwe

No comments:

Post a Comment