Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa na mama yake mzazi katika usafiri wa punda wakati wa mapokezi yake jimboni
Mkazi wa Ludewa akiwa katika maandamano hayo huku akiwa na bango (picha na Francis Godwin
Wananchi wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe wa mapokezi ya mbunge wao Mh. Del Filikunjombe
NA FRANCIS GODWIN IRINGA
VYAMA vya upinzani
wilaya ya Ludewa na mkoa wa
Iringa vimeungana na wapiga
kura wa
jimbo la Ludewa mkoa
mpya wa mkoani Njombe kufanya mapokezi makubwa
ya kihistoria kwa
mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe (CCM) wananchi na
vyama vya upinzini katika jimbo
hilo wakitoa msimamo mzito kwa
chama cha mapinduzi (CCM)
kuwa iwapo kitajaribu
kumfanyia mizengwe mbunge huyo
kwa hatua yake ya aliyoifanya mbunge
Dodoma kwa kusaini fomu ya
kutokuwa na imani ya waziri
mkuu Mizengo Pinda basi jimbo watalikosa.
Wapiga kura hao
wa jimbo la Ludewa ambao
waliungana na vyama vya TLP ,CUF,NCCR Mageuzi pamoja na
wana CCM katika
mandamano makubwa
yaliyoanzia umbali wa
zaidi ya kilometa 10 hadi mjini Ludewa huku
mbunge Filikunjombe akitumia
usafiri wa punda ,walitoa kauli hiyo
jana katika mkutano wa
hadhara uliofanyika viwanja vya michezo
vya Ludewa mjini.
Akizungumza kwa niaba
ya vyama vya
upinzani katika mkutano huo katibu
mwenezi wa TLP mkoa wa
Iringa Branka Haule alisema
kuwa uamuzi wa mbunge
huyo Filikunjombe wa kuweka
sahihi katka fomu iliyoandaliwa na mbunge Zitto Kabwe
(Chadema) kuhusiana na kutokuwa na imani ya waziri mkuu kutokana na baadhi ya
mawaziri wake kufanya
ufisadi wa kutisha ,ni uamuzi uliopokelewa kwa furaha
kubwa na watanzania wote pasipo kujali itikadi zao za
kisiasa .
Hivyo alisema wao kama
vyama vya upinzani wanaungana na hatua ya mbunge Filikunjombe
na wabunge wote
waliopinga vitendo vya ufisadi na utendaji mbovu wa mawaziri
waliotemwa katika baraza
jipya lililoundwa baada
ya wabunge kutangaza kutokuwa na
imani na waziri mkuu Pinda .
Haule alisema wao kama TLP na vyama vyote
vya upinzani ambavyo vinapinga
vitendo vya ufisadi wataendelea
kutoa ushirikiano kwa mbunge
Filikunjombe katika jimbo
hilo la Ludewa na kutokana na hatua ya mbunge huyo
kuonyesha uzalendo kwa umma
bila kuangalia chama chake cha CCM wao
wataendelea kumuunga mkono hata
katika uchaguzi mkuu ujao na iwapo
CCM itajaribu kumfanyia fitina basi
watakuwa tayari kumuunga mkono
popote atakapo kwenda .
Viongozi wa
upinzani walioshiriki maandamano hayo
ni mbali ya Haule ni pamoja na
kampeni meneja mkuu wa mkoa
kupitia TLP mkoa wa Iringa Mrisho Samson , mwenyekiti wa NCCR
Mageuzi wilaya ya Ludewa ,Lazaro Mwinuka , Mwenyekiti wa CUF wilaya ya
Ludewa Asungushe Mtweve, Katibu mwenezi wa TLP
wilaya , Bariki Pangisa , katibu wa wilaya ya Ludewa TLP ,Joseph
Kayombo na katibu wa CUF wilaya ya Ludewa Edwin Mgimba huku
viongozi
wa Chadema wilaya hiyo
wakishiriki wakiungana na wananchi katika mkutano na kugoma
kutambulishwa .
Kwa upande wa CCM
walioshiriki ni pamoja na makamu
mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa
Monica Mchilo, katibu mwenezi wa CCM mkoa Mgaya
pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya na madiwani .
Kwa upande wao wananchi
wa jimbo la Ludewa katika risala
yao iliyosomwa na Casta Mbawala
walisema kuwa wataendelea
kumuunga mkono mbunge huyo
popote atakapokuwa akitetea maendeleo ya
Taifa bila kujali itikadi zao za
kisiasa .
Akiwahotubia
wananchi hao mbunge
Filikunjombe mbali ya kuwapongeza
kwa mapokezi makubwa aliyopata bado alisema kuwa ataendelea kupigania maendeleo ya wilaya ya Ludewa na Taifa kwa ujumla .
No comments:
Post a Comment