Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 13, 2012

Mbunge Filikunjombe apokelewa na mabango ya pongezi jimboni Ludewa ,vyama vya upinzani ,wana CCM wasema wataungana naye popote atakapokuwa



Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa na mama yake mzazi katika usafiri wa punda wakati wa mapokezi yake jimboni
Mkazi wa Ludewa akiwa katika maandamano hayo huku akiwa na bango (picha na Francis Godwin
Wananchi wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe wa mapokezi ya mbunge wao Mh. Del Filikunjombe
NA FRANCIS GODWIN IRINGA
VYAMA  vya  upinzani   wilaya ya  Ludewa na mkoa  wa  Iringa  vimeungana na wapiga kura  wa  jimbo la  Ludewa  mkoa  mpya  wa  mkoani Njombe   kufanya mapokezi  makubwa  ya  kihistoria  kwa  mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo  Filikunjombe (CCM)  wananchi  na  vyama  vya  upinzini katika  jimbo  hilo  wakitoa msimamo mzito  kwa  chama  cha mapinduzi (CCM) kuwa  iwapo  kitajaribu  kumfanyia mizengwe mbunge  huyo kwa  hatua yake ya aliyoifanya mbunge Dodoma kwa   kusaini  fomu ya  kutokuwa na imani ya  waziri mkuu  Mizengo  Pinda basi jimbo watalikosa.
Wapiga  kura  hao  wa  jimbo la  Ludewa ambao  waliungana na vyama vya TLP ,CUF,NCCR Mageuzi  pamoja na  wana  CCM  katika  mandamano makubwa  yaliyoanzia  umbali  wa  zaidi  ya kilometa 10  hadi mjini Ludewa  huku  mbunge  Filikunjombe akitumia usafiri  wa punda ,walitoa kauli  hiyo  jana katika mkutano  wa hadhara  uliofanyika viwanja  vya michezo  vya  Ludewa mjini.


Akizungumza kwa niaba  ya  vyama  vya  upinzani   katika mkutano  huo  katibu  mwenezi wa TLP mkoa  wa Iringa  Branka Haule  alisema  kuwa   uamuzi  wa mbunge  huyo  Filikunjombe wa  kuweka  sahihi  katka fomu  iliyoandaliwa na mbunge  Zitto Kabwe  (Chadema) kuhusiana na kutokuwa na imani ya  waziri mkuu kutokana  na baadhi ya  mawaziri  wake  kufanya  ufisadi  wa kutisha ,ni uamuzi  uliopokelewa kwa  furaha  kubwa na  watanzania wote  pasipo kujali itikadi  zao  za kisiasa .
Hivyo  alisema  wao kama  vyama  vya upinzani   wanaungana na hatua ya mbunge Filikunjombe na  wabunge  wote  waliopinga  vitendo  vya ufisadi na  utendaji mbovu  wa mawaziri  waliotemwa katika baraza  jipya  lililoundwa  baada  ya wabunge  kutangaza kutokuwa na imani na  waziri mkuu Pinda .
Haule  alisema  wao kama TLP na vyama  vyote  vya upinzani ambavyo vinapinga  vitendo  vya ufisadi  wataendelea  kutoa ushirikiano kwa mbunge  Filikunjombe  katika  jimbo  hilo la Ludewa na kutokana na hatua ya mbunge  huyo  kuonyesha uzalendo kwa  umma bila  kuangalia  chama chake cha  CCM wao  wataendelea  kumuunga mkono hata katika  uchaguzi mkuu  ujao na iwapo  CCM itajaribu  kumfanyia  fitina basi  watakuwa tayari  kumuunga mkono popote atakapo kwenda .
Viongozi   wa upinzani  walioshiriki maandamano  hayo  ni mbali ya  Haule  ni pamoja na  kampeni meneja  mkuu  wa mkoa  kupitia  TLP mkoa  wa Iringa Mrisho  Samson , mwenyekiti  wa NCCR Mageuzi wilaya ya Ludewa ,Lazaro  Mwinuka , Mwenyekiti  wa CUF wilaya ya Ludewa  Asungushe Mtweve, Katibu mwenezi  wa  TLP wilaya , Bariki Pangisa , katibu wa wilaya ya Ludewa  TLP ,Joseph Kayombo na katibu wa CUF  wilaya ya Ludewa  Edwin Mgimba huku   viongozi  wa Chadema  wilaya  hiyo  wakishiriki  wakiungana na  wananchi katika mkutano na kugoma kutambulishwa .
Kwa upande wa CCM  walioshiriki ni pamoja  na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya  Ludewa Monica Mchilo, katibu mwenezi wa CCM mkoa Mgaya  pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya na madiwani .
Kwa upande  wao  wananchi  wa jimbo la Ludewa  katika  risala  yao  iliyosomwa na Casta  Mbawala  walisema  kuwa  wataendelea  kumuunga mkono mbunge  huyo popote  atakapokuwa akitetea  maendeleo ya  Taifa  bila kujali itikadi  zao  za kisiasa .
Akiwahotubia  wananchi  hao  mbunge  Filikunjombe mbali ya  kuwapongeza kwa mapokezi makubwa aliyopata  bado  alisema kuwa ataendelea  kupigania maendeleo ya  wilaya ya Ludewa na Taifa  kwa ujumla .

No comments:

Post a Comment