Wakizungumzia mapokezi hayo wananchi hao wamesema kuwa wameandaa mapokezi hayo kwa kushirikiana na vyama vyote vya kisiasa Kama njia ya kuunga mkono ujasiri wa mbunge wao Filikunjombe alioonyesha bungeni kwa kuwa mmoja Kati ya wabunge watatu wa CCM walioungana na wabunge wa vyama vya upinzani kusaini fomu ya kutokuwa na Imani na waziri mkuu Mizengo Pinda na kupelekea baraza la mawaziri kuvunjwa .
Mapokezi hayo yamepangwa kufanyika kuanzia majira ya saa 3 asubuhi kwa wananchi hao kutoka pande mbali mbali za jimbo hilo ambao wametumia usafiri wa pikipiki ,baiskeli na malori kufika eneo hilo la Magereza kwa ajili ya kumpokea mbunge huyo anayetokea jijini D'Salaam .
Mbunge Filikunjombe ameendelea kujizolea umaaarufu mkubwa kutokana na misimamo yake ya kupinga Vitendo vya kifisadi jambo linalomfanya kuwa ni kada na mbunge wa CCM mpambanaji .
Wabunge wote wajifunze kupitia Filikunjombe kuwa ukifanya kile ambacho wananchi wanakitaka utapongezwa na wananchi wote bila kujali itikadi zao. Hongera kaka Deo mapokezi ya leo toka vyama vyote vya siasa na makundi yote ya jamii ni ishara kuwa unafanya kile wapigakura wanataka.
ReplyDeletekweli kaka hillary ingia kwenye blog uone picha za mapokezi aliyopata
ReplyDelete