Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 18, 2012

MWILI WA MCHEZAJI WA SIMBA MAREHEMU PATRICK MAFISANGO WASAFIRISHWA KWENDA NCHINI RWANDA KWA MAZISHI


 Kocha mkuu wa timu ya Simba Milovan Cirkovic akiwa amebeba picha na msalaba wa mchezaji wake Marehemu Patrick Mafisango aliyeafariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia Alhamiswi katika maeneo ya Chang'ombe Veta, wakati mwili wake ulipopelekwa kwenye uwanja wa ndege wa Mawlimi J.K.Nyerere kwa ajili ya kuusafirisha kesho kwenda nyumbani kwao  nchini Rwanda kwa mazishi.
Marehemu Patrick Mutesa Mafisango aliagwa leo kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe na umati mkuwabwa wa mashabiki wa mpira wa miguu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
 Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu wakati alipokewanda kuuaga mwili wa aliyekuwa rafiki yake marehemu Patrick Mafisango aliyeagwa leo.
 Mwili wa marehemu ukiandaliwa tayari kwa kupelekwa uwanja wa ndege ili kuusafirisha kwenda nchini Rwanda mara baada ya kuagwa rasmi leo.
 Makamu Mwenyekiti wa Simba akionekana mwenye majonzi huku akiwa amebeba shada la maua wakati wmili wa marehemu Patrick Mafisango ukiondolewa kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe leo.
 Viongozi pamoja na mashabiki wa timu ya Simba wakiubeba mwili wa marehemu kuupelekwa kwenye gari.
 Mwili wa marehemu Patrick Mafisango ukiingizwa kwenye gari
 Msafara ukielekea uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K. Nyerere.
 Mwenyekiti wa timu ya Simba Ismail Aden Rage akielekeza msafara mara baada ya kufika uwanja  wa ndege.
 Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari  maalum kwa ajili ya kuupeleka kwenye chumba cha  kuhifadhi maiti uwanja wa ndege.
 Gaqri maalum likiupeleka kwenye chumba cha kuhifadhi.
 Mdogo wake marehemu Patrick Mafisango kushoto  ambaye hakutaka jina lake kutajwa akiwa ameshika shada la maua  pamoja na mmoja wa waombolezaji.
Maiti ya Marehemu Patrick Mafisango aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba ukiingizwa kwenye chumba maalum cha kuhifadhia maiti tayari kwa kuusafirishwa kesho kuelekea nchini Rwanda kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment