Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 20, 2012

Roma, Ally Kiba, Dimpoz, AT, Suma Lee, Ben Pol, Barnaba wafunika Tamasha la Kili Tanzania Music Awards Winners Tour Mbeya


 Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana. Kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com
 Suma Lee nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music jijini Mbeya
 Ben Paul nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award jijini Mbeya.
 Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimba jukwaani jana wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine
 Vijana wengi walikuwa wamepigilia vitu vya namna hii
 Mashabiki walikuwa hawatulii
Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba  akiimba jukwaani hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine 
 Wasichana waliokuwa wakitoa huduma ya tiketi
 Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba na Omy Dimpoz katika wimbo Nai Nai jukwaani hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine
Dimpoz kwa Pozi akipitika katikati ya wacheza show wake.
 Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza show wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award  jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana
Back Stage mambo yalikuwa hivi, Toka kushoto ni Ali Kiba, Omy Dimpoz, Ben Pol na Meneja wa Omy Dimpoz Mubenga. Kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com

***********************
MANENO ya Injili yanayosema Wamwisho anakuwa wakwanza na wakwanza akawa wamwisho yametima jana katika Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya pale mkali wa Hip Hop,  Roma  Mkatoliki alipoongoza jahazi la wakali wa Tuzo za Kili Tanzania Musc Awards 2012 katika onesho lao la Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jana.

Roma akipanda jukwaani akisindikizwa na DJ maarufu DJ Choka, alishangiliwa vilivyo na umati wa watu uliofurika uwanjani hapo pale tu ilipofika zamu yake kupanda.

Roma! Roma! Roma! Roma!....hayo ndio yalikuwa maneno ya shangwe kutoka kwa wapenzi wa burudani kutoka Jijini Mbeya waliofurika katika Uwanja wa Sokonine mjini hapa kushuhudia show hiyo kali ya Washindi wa Tuzo za Kili Tanzania Music Awards 2012.

Roma baada ya kumaliza kuimba nyimbo zake kwanza aliwashukuru wana Mbeya kwa kura zao zilizompa ushindi na kuwaambia sasa anamaliza show hiyo ambayo hadi hapo alipofikia alisema wametumia Sh 200/= pekee kati ya Sh 2,000 ya kiingilio waliyotoa.

“Sasa ndugu zangu, nawaambia ukweli hadi sasa mmeshatumia sh 200 tu ya kiingilio chenu,..sasa nawapa show ya Sh 1,800 iliyobaki,” alijigamba Roma ambaye muda wote alikuwa akishangilia na ndipo alipomaliza kwa kuimba Wimbo wa Mathematics uliompa tuzo.

Wasanii wengine waliopanda jukwaani jana ni pamoja na Ben Pol, AT, Ali Kiba , Barnaba, Omy Dimpoz  na Suma Lee nao wamefunika vibaya katika Tamasha la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa sokoine Mjini Mbeya.

Alianza jukwaani kupanda mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B,Msanii Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae alishambulia jukwaa na kuwaamsha watu kuwa sasa show imeanza.

Alifuata jukwaani Suma Lee ambaye aliongozwa na show kali kutoka kwa vijana wake wanne wakike na wakiume na kushangiliwa vilivyo kwa mkongwe huyo wa Bongo Fleva.

Baada ya Ben Pol, alipanda mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT na kutoa burudani ya nguvu na  wimbo wa  Vifuu Utundu ambao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji wake wawili wa kike.

Ikafika zamu ya Omy Dimpoz jukwaani kwa kuimba nyimbo yake mpya ambayo alitaraji kuizindua jana katika Ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam, single ya Baadae kisha  ikafuata ile iliyompa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikiana Nai Nai aliyoanza kuimba peke yake na baadae kuurudia wimbo huo akiwa na Ali Kiba.

Ali Kiba alibaki jukwaani hapo kama ilivyokuwa mjini Moshi na vijana wake kumfuata kutoa shukrani zao za kupata kura zilizowapa ushindi wa tuzo ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa Dushelele.

Wakati mara zote pazia la utoaji burudani kwa washindi hao wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofanya ziara limekuwa likifunga na Roma Mkatoliki akapanda wa pili kutoka mwisho.

Roma ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka na hata alipomaliza show yake bado mashabiki walimtaka aendelee.

Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba ndiye aliyefunga pazia hilo mjini Mbeya kwa kuimba  ikiwapo inayovuma kwa sasa ya Magube Gube.

Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mjini Mtwara na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma na Jijini Mwanza na Moshi.

No comments:

Post a Comment