UBAO WA TAIFA UNAONESHA HIVI
Mchezaji
wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya
kuifungia timu yake goli la kuongoza katika mchezo wa kumaliza michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom inayomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa huku
ikiwa tayari ni mabingwa wa ligi hiyo,
Goli
la pili la Simba limefungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati
na dakika chache zilizopita tayari Emmanuel Okwi ameongeza goli la tatu ,
Juma Kaseja ameongeza goli moja wa penati wakati pia Patrick Mafisango
amefunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika
eneo la hatari
Mchezaji
wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa
Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika leo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi
cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011-2012
kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.
Manahodha
wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa
wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapo.
Picha kwa hisani ya FULL SHANGWE
Wachezaji
wa Simba wakishangilia na Kombe mara baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi
Kuu ya Vodacom iliyomalizika jana Uwanja wa Taifa dhidi ya watani wao wa
jadi Yanga.Simba ilishinda 5-0.
Wachezaji wa Simba wakishangilia na Kombe
Mashabiki wa Simba wakishangilia kwa namna yake
Wachezaji
wa Simba wakitembea mithili ya Simba mara baada ya kuwafunga watani wao
wa jadi Yanga wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.Simba ilishinda 5-0.Mbele ni
Mchezaji wa timu hiyo, Uhuru Selemani na motto wake
Wachezaji wa Simba wakishangilia
Waziri wa Habari akimkabidhi Kombe nahodha wa Simba Juma Kaseja mara baada ya kutwaa Ubingwa timu ya Simba
Mashabiki wakishangilia kwa mbwembwe
Picha zote na Kamanda wa matukio Blog
Picha zote na Kamanda wa matukio Blog
No comments:
Post a Comment