Pages

Saturday, May 19, 2012

TICKET KUWACHEKI CHELSEA NA BAYERN MUNICH UEFA YAUZWA MILIONI NNE.


Allianz Arena, uwanja itakapochezwa fainali ya Eufa kati ya Bayern Munich na Chelsea.
Shaffih Dauda wa Sports Etra na Sports Bar ameripoti kutoka Ujerumani kwamba Ticket za bei rahisi za kuishuhudia mechi ya Chelsea na Bayern Munich Ujerumani May 19 2012 ikiwa ni fainali ya UEFA zimekwisha ambapo ticket pekee zilizobaki ni za Euro 2000 zaidi ya shilingi milioni nne za kitanzania.
Dj Mac ambae ni mbongo anaeishi Munich amesema kwa sasa bado wageni wanazidi kuingia kutoka miji na nchi mbalimbali, hali ya ticket imekua ngumu sana huku pia hata maeneo ya wazi ya kutizama mpira katika screen kubwa nayo yamejaa, mfano Olympia Stadium uwanja wa zamani wa Fc Bayern penye uwezo wa kuchukua watu elfu 30 napo Ticket zimekwisha, na pia sehemu nyingine yenye uwezo wa kuchukua watu elfu 30 kumejaa pia.
Mac amesema Kwa upande wa jezi nazo pia zimepanda sasa hivi zinauzwa kuanzia shilingi laki mbili za kitanzania ambapo mashabiki wa Bayern Munich wamehamasishwa kuvaa jezi nyeupe na nyekundu ambazo zimependezesha mji pia.
Uwanja wa Allianz Arena wakati wa mchana.
kwa hisani ya sport extra na millard ayo

No comments:

Post a Comment