Pages

Wednesday, May 30, 2012

WEMA SEPETU AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA MWINYI WA MACHOZI BAND NDANI YA SUPERSTAR, PICHA ZA USHAHIDI HIZI HAPA!

Wema akikaribishwa kuja kuvishwa pete na Mwinyi ambae amecheza kama Diamond Platnums.
Mwigizaji Wema Sepetu bado anaendelea kuishoot movie yake ya kwanza iitwayo SUPER STAR ambayo inahusiana na maisha yake kwa asilimia kubwa sana, ikiwa ni movie ambayo itaonyesha vitu vingi alivyovipitia kwenye umaarufu wake.
Usiku wa May 29 kuamkia may 30 2012 saa nane na dakika kumi ndani ya Maisha Club Dar es salaam, Wema alivishwa pete na mwimbaji Mwinyi wa Machozi Band ambae kwenye hiyo movie yeye atazicheza nafasi zote za Mwimbaji Diamond Platnums aliyewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu, Mwinyi amecheza kama Diamond ambae pia alimvisha Wema pete ya uchumba hapohapo Maisha Club.

Mwinyi alisema huyu ndio mwanamke nilietulia nae baada ya kuzunguka huko kote na nahitaji awe wangu wa maisha, ni maneno ambayo Diamond aliyasema siku ya kumvisha Wema Pete.
.
Akiongea Exclusive na millardayo.com Wema amesema bajeti ya kutengeneza hiyo movie ni kuanzia milioni 29 mpaka 30 ambapo alianza kuitengeneza march mwaka huu na ataizindua june 23 2012.
Mrembo huyu ambae ni Miss Tanzania 2006 amesema mwanzoni alikua anataka hii movie wacheze Irene Uwoya na Jb na ilikua haikua ikihusu maisha ya Wema lakini baada ya Jb kuwa na kazi nyingi, alifikiria kucheza movie mwenyewe na kupewa idea ya Super Star na msanii Suma Lee.
Alichofanya baada ya kupewa hiyo idea na Suma Lee ni kuipimp na kuongeza matukio mengi aliyokutana nayo kwenye umaarufu na ni movie ambayo mastaa wengi wa kibongo wameuza sura ndani yake.
Wema akivishwa pete.
Yote hii ilikua inarekodiwa na ni sehemu ya hiyo movie mpya ya Wema, sio kweli kwamba Wema na Mwinyi ni wachumba, hapa ni sanaa tu.
.
Ndani la gari la Wema Sepetu akifanya Exclusive interview na Millard Ayo saa tisa kasoro usiku Maisha Club.
.
Millard Ayo kwenye interview na Mwinyi wa Machozi Band Maisha Club.

No comments:

Post a Comment