Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 19, 2012

ALICHOSEMA WAZIRI MEMBE KUHUSU ZILE BILIONI 3 ZILIZODAIWA KUPOTEA.

.
Serikali imetolea ufafanuzi ishu ya pesa ambao ni shilingi bilioni 3.5 ulioidhinishwa na wizara ya mambo ya nje yna ushirikiano wa kimataifa pamoja na utumishi wa umma kwa ajili ya safari ya Rais Jakaya Kikwete kuelekea nje ya nchi, pesa ambazo zilidaiwa kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha  March mwaka huu.
Waziri wa wizara hiyo Bernard Membe baada ya kukutana na washika kalamu amesema fedha zote zimerejeshwa wizarani na kwamba tayari wizara imeunda kamati kuchunguza utaratibu uliotumika kuidhinisha fedha hizo, na kuongeza kwamba wakati wa uidhinishwa wa hizo fedha viongozi wote wa ngazi za juu wa wizara pamoja na muhasibu mkuu hawakuwepo.
Amesema “hizi fedha zote ziliingia kwenye account ya wizara na nyingine zikaletwa wizarani lakini hata senti moja haikuchukuliwa, tuliziona na zikahesabiwa na zilizofika hapa wizarani kwa nia ya safari zilirejeshwa benki kwa hiyo hayupo alieiba, tusimuhukumu mtu ambae hajaiba bado”
Kuhusu ishu yake kwamba amekitabiria chama cha CHADEMA ushindi katika uchaguzi mkuu ujao, Membe amesema  “ni kitu ambacho kiliwekwa makusudi ili kunifitinisha na Chadema na Wanaccm wenzangu nionekana wa ovyo tu nisikaribishe karibishe watu, hamna nitaendelea kukaribisha watu nyumbani kwangu… vijana wa Chadema walikuja kwa heshima zote nyumbani kwangu bahati nzuri walikuja wakati wa mlo wa mchana kama waliotea nikawakaribisha nilikua na marafiki zangu, walifurahi vizuri kweli”

No comments:

Post a Comment