Serikali imetolea ufafanuzi
ishu ya pesa ambao ni shilingi bilioni 3.5 ulioidhinishwa na wizara
ya mambo ya nje yna ushirikiano wa kimataifa pamoja na utumishi wa umma
kwa ajili ya safari ya Rais Jakaya Kikwete kuelekea nje ya nchi, pesa
ambazo zilidaiwa kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha March mwaka
huu.
Waziri wa wizara hiyo Bernard
Membe baada ya kukutana na washika kalamu amesema fedha zote
zimerejeshwa wizarani na kwamba tayari wizara imeunda kamati kuchunguza
utaratibu uliotumika kuidhinisha fedha hizo, na kuongeza kwamba wakati
wa uidhinishwa wa hizo fedha viongozi wote wa ngazi za juu wa wizara
pamoja na muhasibu mkuu hawakuwepo.
Amesema “hizi fedha zote
ziliingia kwenye account ya wizara na nyingine zikaletwa wizarani lakini
hata senti moja haikuchukuliwa, tuliziona na zikahesabiwa na zilizofika
hapa wizarani kwa nia ya safari zilirejeshwa benki kwa hiyo hayupo
alieiba, tusimuhukumu mtu ambae hajaiba bado”
Kuhusu ishu yake kwamba
amekitabiria chama cha CHADEMA ushindi katika uchaguzi mkuu ujao, Membe
amesema “ni kitu ambacho kiliwekwa makusudi ili kunifitinisha na
Chadema na Wanaccm wenzangu nionekana wa ovyo tu nisikaribishe karibishe
watu, hamna nitaendelea kukaribisha watu nyumbani kwangu… vijana wa
Chadema walikuja kwa heshima zote nyumbani kwangu bahati nzuri walikuja
wakati wa mlo wa mchana kama waliotea nikawakaribisha nilikua na
marafiki zangu, walifurahi vizuri kweli”
No comments:
Post a Comment