Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, June 17, 2012

ANDRE VILLA BOAS KUCHUKULIWA NA TOTTENHAM.


.
Kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas amejitokeza kama mmoja wa makocha wanaogombania nafasi ya kuifundisha Tottenham baada ya club hiyo kumfukuza Harry Redknap.
Kocha huyo mreno ambae sasa hivi hana kazi toka february mwaka huu inaaminika kwamba kuna uwezekano mkubwa wa yeye kupata hiyo nafasi baada ya kupata support ya kampuni ya sky bet inayoshughulika sana na ishu za mpira ambao inasemekana jana baadhi ya wakurugenzi wa club hiyo waliwasiliana na villa boas.
Tottenham inamtafuta mrithi wa kocha Harry Redknap ambae ameifundisha club hiyo kwa miaka minne kabla ya kufukuzwa juzi jumatano, Kocha wa Everton  David Moyes na kocha wa Wigan Roberto Martinez wanatajwa pia kwamba wako kwenye hiyo list ya kumchagua mmoja wa kuifundisha tottenham, lakini pia mchezaji wa zamani wa Tottenham Jurgen Klinsmann yuko kwenye hiyo list inayotajwa na vyombo vingi vya habari.

No comments:

Post a Comment