![]() |
Mkwasa |
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu leo.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameiambia BIN ZUBEIRY
usiku huu kwamba ameamua kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia
timu hiyo kutothaminiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkwasa
anachukua hatua hiyo, siku mbili tu tangu timu hiyo itolewe katika
kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika na Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-1 Addis Ababa
na baadaye 1-0 Jumamosi mjini Dar es Salaam.
Mapema
baada ya kufungwa juzi, Mkwasa alisema kwamba timu hiyo haikuwa na
maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa. Lakini Mkwasa
atakumbukwa mno kwa kuifikisha juu timu hiyo, akiiwezesha kushiriki
fainali za Afrika miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini, hiyo
ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.
SOURCE SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment