Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akimkabidhi katibu
wa umoja wa wafanyabishara wa bodaboda msaada wa pikipiki 10.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akizungumza na
wafanyabiashara wa bodaboda (hawapo kwenye picha) muda mfupi kabla
hajawakabidhi msaada wa pikipiki kumi zenye thamani ya shilingi milioni
20.Kushoto ni katibu wa umoja wa wafanyabiashara wa bodaboda, Maulid
Mpondo.Kulia wa kwanza ni Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya
Singida,Williamu Haaly na anayefuata,ni katibu wa CCM manispaa ya
Singida.
Mmoja wa wafanyabiashara wa bodaboda akisoma risala yao kwa mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji.
Waendesha Bodaboda wakimsikiliza mbunge wao.
Baadhi
ya wafanyabiashara wa bodaboda wa mjini Singida wakiserebuka na
kucheza ‘KIDUKU’ na mbunge wao Mohammed Gullam Dewji muda mfupi kabla
ya mbunge huyo kuwakabidhi wafanyabiashara hao msaada wa pikipiki.
Pikipiki
10 aina ya sanlag CC150 zilizotolewa msaada ya mbunge wa jimbo la
Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji kwa vikundi 10 vya wafanyabiashara
wa bodaboda mjini Singida.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji akimkabidhi Mchungaji
Daud Elia mifuko 25 ya saruji kwa ajili ya kujengea kanisa.
Mchungaji
wa kanisa la Pentekoste kijiji cha Ititi akitoa nasaha zake muda mfupi
kabla ya kumkaribisha Mo kuzungumza na waumini wa kanisa hilo.
Mo
akizungumza na waumini wa kanisa la Pentekosti la kijiji cha Ititi
muda mfupi kabla hajakabidhi msaada wa mifuko 25 ya saruji na shilingi
laki tano taslimu.
Jengo la kanisa la Pentekoste la kijiji cha Ititi jimbo la Singida mjini.
Na Geofrey Mwakibete na Nathaniel Limu
Wafanyabiashara
wa bodaboda jimbo la Singida mjini,wamehimizwa kuunda/kuanzisha
vikundi ili pamoja na mambo mengine, kujijengea mazingira mazuri ya
kukopesheka.
Wito
huo umetolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam
Dewji,wakati akizungumza kwenye hafla iliyofana, ya kukabidhi pikipiki
10 aina ya sanlag CC 150 zenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa
vikundi vya wafanyabiashara wa bodaboda.
Alisema
faida za kujiunga kwenye vikundi ni nyingi ikiwemo ya kuwa nafasi
nzuri ya kupata mikopo mbalimbali kutoka kwenye taasisi za kifedha.Mtu
mmoja mmoja akitaka kukopa fedha benki ni ngumu, kuotokana masharti
yaliyowekwa na taasisi za kifedha.
“Siku
zote umoja ni nguvu,utegano unachangia kuleta ulegevu unaozaa
udhaifu.Mahali pana ulegevu,kwanza hakuna maendeleo ya kweli na pia
kutetea haki,inakuwa ngumu mno”,alifafanua Dewji ambaye pia ni mjumbe wa
NEC CCM mkoa wa Singida.
Kuhusu
pikipiki hizo alizotoa msaada, alisema lengo lake ni kwamba kila
kikundi kitaitumia pikipiki yake kwa ajili ya kukiongezea kikundi mapato
ambayo endapo yatatunzwa vizuri,ipo siku kila mwanakikundi anaweza
akamiliki pikipiki yake binafsi.
Aidha,
amewataka wakati wote kuzingatia sheria halali zilizowekwa na mamlaka
husika, ili shughuli zao ziweze kuendelea bila matatizo.
“Pia
napenda kutumia fursa hii, kuomba mamlaka zinazohusika na sheria za
usalama barabarani na utozaji wa kodi na ushuru, kujipanga kwa ajili ya
kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa bodaboda,ili waweze kuzifahamu
sheria husika”,alisema na kuongeza;
“Nina
imani kwamba wafanyabiashara wa boda boda wakifahamu kwa kina sheria
za usalama barabarani,kutapunguza mno ajali na pia wakifahamu mambo ya
kodi na ushuru,hawatakwepa kulipa”.
Katika
hatua nyingine, Dewji amewahimiza waumini wa madhehebu ya dini,
kuongeza kasi ya utoaji sadaka,ili kuimarisha ustawi wa madhahebu yao.
Alisema
waumini wanao wajibu mkubwa wa kuchangia kwa hali na mali madhehebu
yao kwa lengo yaweze kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi zaidi.
“Sadaka
inayotolewa kwa moyo mkujufu,licha ya kusaidia ustawi wa dhehebu la
dini husika,mtoaji anakuwa amejiwekea thawabu mbele ya mwenyezi
Mungu”,alisema Dewji.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo,mbunge huyo, alisema ustawi wa kweli wa dhehebu
la dini,utaletwa na waumini wenyewe,watu wengine/taasisi zingine,kazi
zao ni kusaidia mahali waumini wanapokuwa wamepelea.
Katika
siku yake ya pili ya ziara yake ya kikazi jimboni kwake,Dewji alitoa
msaada wa mifuko ya saruji 40 kwa msikiti wa kijiji cha Manguamitogho na
mifuko mingine 25 ya saruji na shilingi laki tano taslimu, kwa kanisa
la Pentekoste la kijiji cha Ititi.
Katika
siku yake ya mwisho ya ziara yake (17/6/2012),Dewji alitarajiwa kuwa
na kikao maalum na madiwani wa kata za Singida mjini,kuzindua kisima
cha maji cha kijiji cha Mtisi,kuzungumza na wanachama wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Singida na kukagua kituo cha afya cha
Sokoine mjini Singida
No comments:
Post a Comment