Roberto Di Matteo
Chelsea hatimaye imemteua Roberto Di Matteo kama meneja wake wa kudumu kwa kutiliana saini mkataba wa miaka miwili.
ashinda FA na Ulaya
Di Matteo aliwekwa kama kocha wa mda
kufuatia kutimuliwa kwa Andre Villas-Boas mnamo mwezi Machi, na akaweza
kuiongoza klabu hio akifanikiwa kuifikisha na kushinda fainali ya Ligi
ya Mabingwa wa Ulaya na vilevile kombe la FA la England.
Meneja huyo aliyekua kiongozi wa MK
Dons na pia West Brom, Di Matteo alipoteza mechi tatu tu kati ya mechi
21 alizosimamia, na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu
waliunga mkono ateuliwe kama meneja wa kudumu hususan baada ya kushinda
kombe lililoikwepa klabu hio kwa mda mrefu la Mabingwa wa Ulaya
No comments:
Post a Comment