Mwimbaji
staa wa Tanzania Diamond Platnums ambae alitangaza kwamba mwaka huu
utakua wa kolabo atakazofanya za wasanii wengine, amesema huo mpango
unakaribia kufikia mwisho. “sikuwahi kufanya kolabo sana mwanzoni kwa
sababu nilitaka kuonyesha watu uwezo wangu kwanza, baada ya hapo ndio
nikaamua kufanya kolabo ambazo sasa naelekea kuzisitisha na nyingine
nimefanya mpaka na wasanii wa nje ya Tanzania, mpaka sasa zimefika nane
na nilitaka kumi tu na ninafikiria hizo mbili zilizobaki nifanye zangu
tu” – Diamond Platnums. Kuhusu ishu ya kumchaji msanii anaehitaji
kolabo nae, Diamond amesema “kiukweli inategemea uhusiano wangu na wewe
lakini kama hatujuani, kama umekuja kibiashara kwa sababu muziki ni
biashara utalazimika kunilipa milioni tano kama ni verse na Chorus
itakua milioni kumi nafanya na Video pia, muziki umebadilika sasa hivi
kwa sababu kwenye show watu wanakula milioni 5, 7 mpaka kumi” Mpaka
sasa Diamond amesema hajawahi kumchaji msanii yeyote pesa kwa ajili ya
kolabo lakini hicho ndio kiwango alichojiwekewa yakitokea mazingira kama
hayo.
WAZIRI WA IRELAND AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI , ATEMBELEA DIT
-
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland anayeshughulikia Ushirikiano
wa Kimataifa, Maendeleo, na Diaspora, Mhe. Neale Richmond, amehitimisha
ziara ya...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment