Pages

Wednesday, June 27, 2012

Gazeti la Italia lamfananisha Balotelli na ‘King Kong’



MARIO BALOTELLI amejikuta katika kasheshe jingine la ubaguzi wa rangi baada ya gazeti la michezo linalouza na kusomwa zaidi nchini Italia kumfananisha na KING KONG (Gorilla).
Gazeti hilo la asubuhi ‘Gazzetta dello Sport’ lilichora picha ya Balotelli akiwa juu ya jengo refu kwa kuigiliza scene ya filamu ya King Kong alipokuwa amepanda kwenye jengo refu la New York la Empire State.
Picha hiyo iliyochorwa na mchora katuni Valerio Marini inaashiria jinsi Balotelli alivyoitawala Uingereza.
Hata hivyo maelfu ya wasomaji wenye hasira wameilaani picha hicho kwa kuonesha ubaguzi wa rangi dhidi ya Balotelli, ambaye wazazi wake walizaliwa nchini Ghana, na hivyo Gazzetta kulazimika kuomba radhi.
Gazeti hilo la mjini Milan limekiri kwa kusema: “Tunahitaji uangalifu zaidi na tahadhali.”
Balotelli ni mshambualiji wa Manchester City ya Uingereza na pia mchezaji wa timu ya taifa ya Italia.

                             SOURCE BONGO 5

No comments:

Post a Comment