Pages

Saturday, June 23, 2012

KASHFA NZITO: Maiti ya kichanga yayeukia Mwananyamala, katibu wa hospitali ageuka bubu


Mwananyamala Hospital katika kashfa nyingine
Katika hali ya kushangaza, maiti ya kichanga kilichozaliwa kikiwa tayari kimefariki, imeyeyukia katika Hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es salaam, ambako mama aliyejifungua alikuwa amepelekwa kujifungua.
Kwa mujibu wa maelezo kuhusu kashfa hii ya aina yake, mama aliyepoteza mtoto wake, alifika hospitalini hapo baada ya kushikwa na uchungu ambapo alijifungua salama, lakini kwa bahati mbaya mtoto huyo hakuwa riziki, na alishafariki.
Mama mzazi akakubaliana na maumivu ya uchungu pamoja na hali halisi kuwa maandiko ya Allah yalishatimia. Lakini wauguzi katika Hospitali ya Mwananyama wakaona kuwa vipigo hivyo havijamtosha mwanamke wa watu, wakaamua kufunga kazi kwa kuupotezea kusikojulikana mwili wa kichanga chake.

No comments:

Post a Comment