Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, June 16, 2012

KIJANA JACKSON THOBIAS a.k.a KUSH, AFARIKI KWA KUGONGWA NA TRENI-KIPAWA AKISIKILIZA MUZIKI KUPITIA HEADPHONES


 Kijana Jackson Thobias, enzi za uhai wake.

Na.Mwandishi wetu.
Imeelezwa sababu za kifo cha kijana huyu ni kutembea katika njia ya Reli, huku akiwa anachati na simu yake ya mkononi, huku akisikiliza muziki kupitia Head phone za simu na kumfanya kutosikia kelele na Treni hiyo hadi ilipomgonga.

Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias, aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na Treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza muziki kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group  ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition  wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.

2 comments:

  1. Inabidi vijana tuwe makini zaidi tuwapo barabarani maana kwa style hii watagongwa wengi.

    ReplyDelete
  2. kweli kaka mana vijana siku izi ndo imekua style

    ReplyDelete