Bwana
Alex Mwaipasi katibu Mkuu wa chama cha kuogelea akizungumzia maonyesho
yatakayokuwa maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya jinsi ya kutumia maji
wakiwa salama ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kujiokoa unapopata
dharura ya kuzama kwenye maji kushoto ni John Belele Mwenyekiti wa chama
cha kuogelea, Maonyesho hayo yatafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika
International School Upanga jijini Dar es salaam kuanzia Juni 27-29
TAARIFA YA CHAMA CHA UOKOAJI
Tanzania
Life Saving Society (TALISS) ni taasisi ya kitaifa isiyo ya kiserikali
ambayo jukumu lake kubwa ni kuzuia/kupunguza idadi ya vifo
vinavyosababishwa na maji, kwa njia ya kutoa elimu kwa jamii jinsi ya
kuishi salama karibu/ndani ya maji, pamoja na kusimamia maswala ya
usalama kwa watumiaji wa maji ya wazi (Open water) na mabwawa (Swimming
pools).
Katika
kuendelea kutimiza wajibu wa kuelimisha jamii, Tanzania Life Saving
Society (TALISS), kwa mara ya kwanza inazindua Wiki ya Kuzuia Vifo
Katika Maji Kitaifa (NATIONAL DROWNING PREVENTION WEEK) utakaofanyika
katika shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST) iliyopo upanga Dar es
salaam, kuanzia tarehe 26mpaka tarehe 30 Juni, 2012 kila siku
saa 8:00 mchana mpaka saa 11:00 jioni, sambamba na hilo TALISS pia
itakuwa inaadhimisha miaka 20 ya kuzaliwa kwake.
Katika
uzinduzi huo tutatoa semina na kufanya maonesho mbalimbali, ambapo
kusudi kuu la tukio hilo ni kukuza na kueneza elimu ya uokoaji na
usalama katika maji hapa nchini.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu.
Wako katika uokoaji wa maisha,
ALEXANDER H. MWAIPASI
KATIBU MKUU
|
No comments:
Post a Comment