Habari
za Hivi Punde kutoka Kijiji cha Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro zinadai kuwa Mashamba ya wananchi yaliyo na Minazi, Migomba,
Miwa na Mazao mengine ya kudumu yaliyo porwa na Mwekezaji wa Kizungu
kwa kuzungushiwa uzio yanateketea kwa Moto mkubwa. Chanzo cha Moto huo
inasemekana ni Walizi wa Mzungu huyo ambao huingia shambani humo mara
kwa mara na kuiba mazao mashambani humo ndio wamesababisha moto huo
ambao utaleta hasara kubwa.
Hivi
Karibuni Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Michezo na Vijana , Amos Makala aliitisha Mkutano wa kutatua Mgogoro huo
uliodumu kwa miaka miwili sasa lakini Mkurugenzi wa Mvomero aliahirisha
Kikao hicho kwa madai ya kuambiwa na DC wa Mvomero hadi alijue tatizo
hilo kwa undani ndipo ashiriki Mkutano na Wananchi.
Kuchomwa kwa mashamba hayo huenda kukaleta mzozo mkubwa baina ya wananchi na Mwekezaji huyo.
No comments:
Post a Comment