Pages

Friday, June 15, 2012

MATUKIO YA TUZO ZA MWANAMICHEZO BORA WA TASWA JANA USIKU DIAMOND JUBILEE

Mpiga picha wa ITV Noel Kapanda akiwa kazini
Mpiga Picha wa ITV Fanuel Mgonja
Mpiga Picha wa ITV Idd Salum akiwa kazini

Baba mwenye uzao wa mabondia Mzee Matumla kulia  akikabidhi tuzo ya mwanamchezo bora wa kigeni katika soka Emmanuel Okwi kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya mchezaji huyo, katika tuzo  zinazoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Agrey Morris katika hafla hiyo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Coast Union ya Tanga na Timu ya taifa Salim Amir akikabidhi tuzo kwa mchezaji Shomari Kapombe 
Mpiga picha wa siku nyingi Athmani Hamisi akikabidhi tuzo kwa mchezaji bora wa kiume katika mchezo wa VoliboMbwana Ally huku akisaidiwa na msaidizi wake
Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za TASWA Masoud Saanane akizungumza katika hafla ya utozi wa tuzo hizo usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwanamichezo bora wa Tanzania.Picha Kwa Hisani Ya Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment