Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, June 25, 2012

MBARONI KWA KUMCHINJA NA KUMUUA MKE WAKE



Na. Luppy Kung’alo, Jeshi
la Polisi Dodoma.

  Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linamshikilia mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel s/o Lusega miaka (42) kabila mkaguru na
mkazi wa Morisheni kata, tarafa na wilaya ya kongwa kwa tuhuma za kumchinja mke
wake na kumuua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. ZELOTHE STEPHEN
alisema Tukio hilo limetokea tarehe 25/06/2012 muda (08:00hrs) wa saa mbili
asubuhi leo, katika eneo la Morisheni Kata, Tarafa na Wilaya ya Kongwa.
“Mtuhumiwa alikwenda
kuripoti mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kongwa kuwa amemchinja
na kumuua mke wake kwa sababu hamsikilizi.” alieleza Kamanda Zelothe.
Bw, Zelothe alisema
mtuhumiwa huyo wakati anaripoti tukio hilo katika kituo cha Polisi alikuwa na
barua mkononi ikieleza madai hayo kwa marehemu mke wake, ikiwa na anuani
ikielekeza kwa Afisa Usalama wa wilaya ya Kongwa, lakini barua hiyo ameikabidhi
katika kituo cha Polisi.
Kamanda ZELOTHE STEPHEN
alimtaja mwanamke huyo aliyeuwawa kuwa ni Telophena w/o Machimo umri miaka (34)
kabila Mkaguru, muuza mgahawa  na Mkazi
wa Morisheni wilayani kongwa
Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema   askari walikwenda kukagua eneo la tukio na
kukuta marehemu amechinjwa kwa kukatwa koromeo na akiwa katika dimbwi la damu
pamoja na kisu kilichotumika kikiwa kando yake.
Kamanda huyo wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Dododma alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwa
kuwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kwa kutembea nje ya ndoa pia kwa
kutoleta matumizi ili hali merehemu ni muuza mgahawa katika eneo hilo
Hata hivyo Kamanda Zelothe
alisema mtuhumiwa huyo ana historia ya ugonjwa wa akili kwa mujibu wa maelezo
ya wanandugu na viongozi wa kijiji wa eneo hilo.
Mtuhumiwa amekamatwa na
anashikiliwa katika kituo cha Polisi Wilayani Kongwa na  atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo
mkabili, alisema Bw. Zelothe.

No comments:

Post a Comment