Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, June 23, 2012

MTOTO ALIYENG'ATWA NA SIMBA KWENYE ZOO HUKO TEGETA


Awali ya yote huyu mtoto na dada yake wa miaka nane na aunty yake waliamua kufunga safari kwenda kwenye zoo kama kutalii tu.Kufika kule wakalipia na kufata taratibu zote za kuingia humo.Wakawa wanatembea wenyewe bila mtu wa kuwaongoza.Aunty waliyekuwa nae ambae ni mkubwa akawa ameenda chooni kujisaidia.
Huyu mtoto ni mtundu sana akawa ameona simba yupo kwenye cage akaenda akafungua  mlango akawa anataka kumshika simba.Mwenyewe anasema alikuwa anataka kumshika kidevu,usoni na kichwani.Ndio simba kumparua kama unavyomuona pichani.Akaja dada mtu mwenye miaka nane akawa anamvuta mkono kumuokoa huku akipiga kelele.Kelele zikamfikia baba mwenye asili ya kiasia ndio kuja mbio kumpiga simba mawe simba akarudi nyuma na kumtoa mtoto.
Baada ya hapo wakampeleka hospitali kwa matibabu na mpaka sasa anaendelea na matibabu nyumbani.Malalamiko yao ni kwa nini zoo yao haina ulinzi wa kina kwa watu wanaoenda hapo?toka mtoto wao amejeruhiwa na simba wamiliki hao hawajawahi hata kwenda kumjulia hali mtoto wao.

No comments:

Post a Comment