Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, June 3, 2012

NSAJIGWA ASEMA HATAOMBA MKATABA MPYA YANGA


Shedrack Nsajigwa mwenye jezi ya kijani.

Nahodha wa Taifa Stars Shedrack Nsajigwa ambae alikua akiichezea club ya Yanga amesema haitatokea hata siku moja akaomba mkataba mpya Yanga kwa sababu anajiamini yeye ni mchezaji mzuri.
Amesema “mimi mkataba wangu na Yanga umeshaisha kwa hiyo mimi ni mchezaji huru, nilijua siwezi kuwepo  Yanga milele… mkataba umeisha naangalia mambo mengine kwa sababu nilisaini mkataba wa miaka miwili nikijua siku moja nitaondoka”
Kuhusu yeye kuomba mkataba mwingine baada ya aliokua nao kumalizika, Nsajigwa amesema “mimi ni mchezaji bwana najiamini na kazi yangu, siwezi kuomba mkataba bado nguvu ya kufanya kazi ninayo siwezi eti kuomba mkataba na timu fulani, aaah never…. sijawahi na haitatokea”
Inaaminika kwamba Nsajigwa ametemwa Yanga kwa sababu alikua kiongozi wa wachezaji wenzake kugoma kwa kudai malipo yao, stori nyingine ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Club hiyo inampango wa kuwaondoa wachezaji wote wenye umri mkubwa na kutaka damu changa kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment