Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 27, 2012

SIMBA YAMTEMA RASMI JUMA JABU, HARUNA ATOLEWA KWA MKOPO

Juma Jabu
KLABU tano za Ligi Kuu ya Tanzania zimewasilisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) majina ya wachezaji ambao zimewakatishia mikataba/mikataba yao kumalizika au kuwaacha kwa ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa 2012/2013.
Kwa mujibu wa klabu hizo, wachezaji waliomaliza mikataba Simba kwa mujibu wa klabu hiyo ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago, Juma Jabu wakati Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu, wakati wachezaji ambao inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina. 
Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11. Azam imekatisha mikataba ya wachezaji watatu.
Wachezaji 12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar wakati wakati kwa upande wa Simba wachezaji waliomaliza mikataba ni wanne huku ikionesha nia ya kuwatoa kwa mkopo wengine wanne.
Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment