Afisa utetezi wa matukio ya mauaji
ya Albino kutoka Shirika la Under the Same Sun Bw, Kondo Seif akiongea
na waandishi wa habari leo katika ofisi za Shirika hilo linalohusika na
kutetea Maalbino nchini juu ya mauaji ya Albino yanayoendelea kutokea
nchini Tanzania. Bw. Kondo alisema kuwa wanasikitika na kufadhaishwa na
mauaji ya mwanaume asiyetambuliwa kati ya umri wa miaka 25-35 mwenye
ulemavu wa ngozi yualiyofanyika katika kijiji cha nambala kata ya Kikwe
Tarafa ya Mbuguni wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha . Alisema kuwa
wamekuta mwili wake ukiwa umeharibiwa vibaya na kwamba ulikuwa
umen'golewa sehemu kadha za viungo vya mwili wake vikiwemo mikono,
masikio, ulimi,ngozi ya usoni,sehemu za makalio na sehemu zote za nyeti
zake na nywele za kichwani. Alisema kuwa mwili wake umehifadhiwa katika
hosipitali ya Mkoa Mount Meru. | |
No comments:
Post a Comment