skip to main |
skip to sidebar
VENGU ATUA BONGO, AFICHWA
Na Mwandishi Wetu
MUNGU mkubwa lakini madaktari wa Kihindi nao ni noma! Ndivyo alivyoanza
kusimulia shuhuda aliyemuona staa wa Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba
‘Vengu’ anayedaiwa kutua Bongo kwa siri na kufichwa, Amani limeinyaka.
ALIYEMUONA
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, Vengu aliyekuwa akitibiwa
maradhi ya kichwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India tangu mwaka
jana, alitua Bongoland hivi karibuni na kufikia nyumbani kwao maeneo ya
Mabibo jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Vengu ambaye alilazwa
Hospitali ya Muhimbili tangu Agosti, mwaka jana na baadaye kuhamishiwa
India baada ya hali kuwa tete, tangu atimbe nchini amekuwa akifanyishwa
mazoezi ya kutembea kwa siri.
“Kuongea anaongea lakini siyo vizuri sana, inaelekea ulimi ni mzito.
Mtu ukilazwa karibia mwaka mzima bila kuongea huwezi kunyanyuka tu na
kuongea,” alisema shuhuda huyo.
USIRI
Katikati ya Mei, mwaka huu ilidaiwa Vengu angerejea nchini
wakati wowote baada ya afya yake kutengemaa lakini ndugu mmoja wa karibu
(jina lipo) alisema walipindisha taarifa na kumleta kwa siri kupitia
mlango wa VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar.
WENZAKE WANASEMAJE?
Amani lilizungumza na wachekeshaji wenzake juu ya kutua Bongo ambapo baadhi walikiri na wengine kudai hawajui chochote.
SEKI VIPI?
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Orijino Komedi, Sekioni
David ‘Seki’ alipopigiwa alisema kuwa hawezi kuthibitisha lolote hivyo
Amani liwatafute ndugu wa staa huyo.
AHAMISHIWA KIMARA
Alipotafutwa ndugu wa staa huyo, alidai kuwa
kweli Vengu yupo Bongo lakini alihamishwa Mabibo na kupelekwa Kimara,
Dar anakoishi na shangazi yake kwa sasa akiendelea na mazoezi ya
kutembea.
TURUDI NYUMA
Vengu alikuwa akikabiliwa na ugonjwa uitwao Brain au
Cerebral Atrophy. Ugonjwa huu husababisha seli za kichwani kukosa
mawasiliano na sehemu nyingine na mgonjwa huzimia mara kwa mara.
SOURCE GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment