WAKAZI
wa Kata ya Kiluvya B Kisarawe Mkoani Pwani, wamemtuhumu Diwani wa Kata
hiyo Azamen Massawe, kwa tuhuma za kujipa tenda ya ujenzi ofisi ya kata
kinyume cha taratibu za tenda kinavyotakiwa.
Wakizungumza
na na Fullshangweblog kwa nyakati tofauti jana wakazi hao walidai kuwa, wanashangazwa
na hatua ya diwani huyo ya kujibebesha tenda kimya kimya bila
kuitangaza kwa wazabuni wengine jambo ambalo halikubaliki.
Walisema kuwa ujenzi wa ofisi hiyo, mbali na kufanyika kimya kimya lakini wanautilia
shaka kutokana na utaratibu mbovu wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi uliotumika kwani haukufuata sheria.
Walifafanua
kuwa ujenzi huo uligharimu shil. milioni 24 ambapo wakazi hao
wanapinga, kutokana na nguvu kubwa ya ujenzi huo imetokana na wananchi
wenyewe.
Wakazi hao
waliongeza kuwa licha ya ubadhilifu uliofanywa diwani huyo,bado vifaa
vingi vilivyotumika katika ujenzi huo vimetoka katika duka lake la vifaa
vya ujenzi.
“Awali
alituuzia matofali ambapo kila moja liligharimu shil. 2500 huku akidai
kuwa ofisi hiyo imetumia nondo 162 jambo ambalo si kweli, kwa sababu
mosi ofisi hiyo tumeijenga sisi wenyewe kuanzia msingi” walisema kwa
jazba wakazi hao.
Naye
diwani wa kata hiyo Massawe, alipotakiwa kutoa ufafanuazi juu ya sakata
hilo alisema hivi “ cha msingi mimi ni mfanyabiashara hivyo sikuona
vibaya kuchukua tenda hiyo, na gari langu ndilo lililotumika kupeleka
vifaa vya ujenzi katika ofisi hiyo bure bila malipo.
Vile vile
alidai kuwa kamati ya ofisi iliyoratibu shughuli zote za ujenzi ndio
inayoweza kuzungumzia suala hilo kwa kina kwa sababu ilihusika moja kwa
moja katika mchakato mzima wa ununuzi wa vifaa.
SOURCE FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment