Pages

Friday, June 15, 2012

Wanafunzi wafanya vurugu kwa kukosa UBWABWA shule ya Seminari Manow


 Askari Kanzu akipita katikati ya wanafunzi kuwanasua wale wanaotajwa kuongoza vurugu hizo.
 Mitihani ambayo ilikuwa ifanywe na wanafunzi hao kesho ikiwa imechanwa chanwa na kutapakaa katika maeneo ya shule hiyo.
 Miongoni mwa uharibifu walioufanya wanafunzi hao kwa madai ya kukosa ubeche shuleni hapo ni pamoja na kuvunja vunja madisha yote ya shule hiyo na ofisi za walimu kama inavyoonekana.
 Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya Chrispine Meela akizungumza na wanafunzi wa shule ya Manow baada ya kutokea kwa vurugu hizo.
Mkuu wa Wilaya akiwa pamoja na Uongozi wa shule hiyo na Kanisa. 
**************
Na Ally Kingo, Rungwe
Wanafunzi 24 wa Shule ya Seminary Manow, Iliyopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi kufuatia  vurugu na uharibifu wa mali za shule na kanisa zilizotokea usiku wa Juni 13,2012 shuleni hapo.

Wanafunzi hao wanatuhumiwa kufanyafanya uharibifu wa mali ya shule hiyo huku vitu vingine vikiibiwa  na jumla ya thamani ikitajwa kuwa ni Shilingi Milion 50.

Akiongea na Father Kidevu Blog, Mkuu wa Shule hiyo ya Manow, Watson Masiba amesema kuwa mgomo huo ulianza mchana kwa kuwa wanafunzi hawakutaka kula Ugali bada ya uongozi kuwaarifu kuwa siku hiyo hakutakuwa na ratiba ya wali kwa kuwa mchele siku hiyo ulikuwa kidogo stoo.

Uongozi wa shule ulipojitahidi kusuruhisha suala hilo kwa kaandaa chakula hicho usiku huo lakini wanafunzi hao walianza kufanya vulugu kwa kuvunja vioo vya majengo na kuvunja milango na kuiba computa 11 za shule pamoja na kuingia katika chumba cha kuandalia mitihani na kuchana mitihani yote iliyo andaliwa kwa ajili ya kuanza kuifanya hapo kesho tarehe 15.06.2012.

Kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi na wana kijiji wanao izunguka shule hiyo imejionyesha kuwepo kwa tofauti kati ya uongozi wa shule na wanafunzi hivyo kufikia wanafunzi hao kutafuta sababu ya kufanya vurugu kwa kiasi cha uharibifu wa mali za shule na Kanisa.

Nae Askofu Dr Esrael Mwakyolile amesema kuwa uharibifu ni mkubwa sana na zaidi ya mali zisizo pungua shiringi milion 50 zimeharibiwa hivyo ameitaka serikali kupitia vyombo vya dola kuchukua hatua kwa wale watakao bainika kuhusika na tukio hili kulipa fidia pamoja na kuwa uongozi wa shule utawachukulia hatua za kinidham.

Naye mkuu wa Wilaya ya Rungwe Chrispin Meela kwa kushirikiana na kamati yake ya ulinzi na usarama amekemea vikali kitendo kilicho fanywa na wanafunzi hao ukizingatia shule hiyo ni ya kanisa la kiinjili la Kilutheri hivyo kuwa mfano wa tabia njema kuliko kuchukua hatua za Kigaidi kuharibu majengo na kuiba mali za shule.

Bwana Meela amechumkua hatua ya kuifunga shule hiyo hadi tarehe 02.07.2012 kwa kidato cha pili, tatu, Nne na sita kwa kuwa imeonekana kuwa ndio viongozi wa uharibifu huo na wanafunzi wajapo shuleni hapo waje na wazazi wao na maelezo binafsi kwa barua.
Jeshi la Polisi limeweka doria shuleni hapo na kuimarisha ulinzi.

No comments:

Post a Comment