Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 8, 2012

BAADA YA MORRISON, POGBA SASA NI FRYERS - KWANINI MAN UNITED WANAPOTEZA MATUNDA YA ACADEMY YAO?



Ravel Morrison alikuwa wa kwanza kuondoka. Paul Pogba sakata la uhamisho wake  kwenda Juventus limemalizika wiki iliyopita rasmi baada ya Ferguson kuthibitisha ameenda Juve. Sasa jina jipya la mchezaji kinda kutoka kwenye academy ya United, Zeki Fryers  ambaye nae anakaribia kutua Tottenham Spurs. Kwanini Manchester United wanapata wakati mgumu kukaa kwa muda mrefu na wachezaji wake wa kutka kwenye academy yao.
Kwa klabu ambayo imepata mafanikio makubwa na mfumo wa kuingiza wachezaji makinda kutoka kwenye Academy mpaka kwenye timu kubwa ni vigumu kuelewa kwanini hivi karibuni wanashindwa kudumu na makinda yao.

Itakumbukwa kauli ya Alan Hansen alyomwambia Ferguson: "Huwezi kushinda chochote na wachezaji watoto." Na Fergie akafanya kinyume chake na kushinda makombe mengi sana na kikosi kilichoitwa cha watoto kilichowahusisha wachezaji kama Ryan Giggs, Scholes, Beckham na wengine wengi.

Kwenye kipindi cha hivi karibuni United ambao wamepata mafanikio makubwa kupitia mfumo wa wa kukuza vipaji - wamekuwa wakipoteza wachezaji wao makinda ambao wanaonekana kuwa na vipaji vikubwa.

Kwanini mchezaji mwenyewe akataka kuondoka? Tena kwnye klabu inayosadikika kuwa maarufu, yenye mashabiki wengi, mafanikio na tajiri kuliko - huku akiwa na uhakika kupata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Yote haya yamepafanya Old Trafford kuwe sehemu nzuri kwa wachezaji. Kila mtu alilijua hili. Labda hilo ndio lilikuwa tatizo.

Wachezaji wadogo kama Pogba wamekuwa wakichanganywa akili na mishahara mikubwa inayotolewa na vilabu vinginena United wanakuja kugundua kwamba brand ya Red Devils haina ushawishi mkubwa kama iliyokuwa nayo mwanzoni. Kuna taarifa kwamba Pogba alihadiwa kwamba kuanzia msimu wa 2011-2012 angekuwa anapata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza lakini mwishowe akaishia kupata kucheza kwenye mechi 7, huku tatu zikiwa kwenye mechi za kombe la Carling.

Ahadi ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza ilikuja kuonekana imetimizwa kwa kiasi kidogo sana. Pogba hakuwa tayari kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya jezi ya United na akaamua kubadilisha upepo kwenda Turin.

Pamoja na matatizo mengine lakini hili na nafasi ya kucheza mara kwa mara limechangia kwa makinda kushindwa kuendelea kubaki Old Trafford.

Wakati hakuna mchezaji anayepaswa kulipwa kulikovile anavyostahili, lakini kuendelea kukataa kuafikiana na wachezaji wake makinda ambao wana vipaji vikubwa kunaweka hatari kubwa kwa klabu hiyo yenye mafanikio makubwa kwenye premier league.

Pogba na Morrison ni vijana ambao walikuwa wakitajwa kuwa ndio nguzo ya miaka kadhaa ijayo ya  safu ya kiungo ya United, walikuwa ndio watakaokuja kuwa waokozi wa safu hiyo ambayo kwa kwa siku za hivi karibuni ndio imekuwa sehemu yenye udhaifu kwenye kikosi cha Red Devils, lakini badala ya kuendelea kuwashikilia vijana waliowakuza huku akitafuta top layers wa muda - United wameacha makinda yao yaondoke huku wakimuachia msala wa kutafuta wachezaji wa bei chee Fergie.

Lakini chini ya utawala wa Glazers United wamekuwa wakishindwa kufanya usajili wa wachezaji wakubwa kutokana na bei pamoja mahitaji binafsi ya wachezaji, mfano mzuri ni akina Wesley Sneijder, Samir Nasri, Eden Hazard na hata hivi sasa Modric anaweza akaongezeka kwenye listi. Hivyo kutokana na kuwa wanyonge kwenye kushindana na timu aina ya Real Madrid, Barelona, Chelsea na City njia rahisi katika kuweza kuendelea kupata wachezaji wazuri ni kupitia mfumo wa wachezaji vijana.




Mahasimu wao Manchester United wanaweza kuja kutamba kuwashinda wengi kwa ubora wa wa academy yao ya kitajiri iliyo njiani, lna huku United wakiwa hawana uwezo wa kushindana na nguvu ya matumizi ya Noisy Neighbours - hivy bado njia nzuri zaidi ya kushindana nao na kuboresha mfumo wao mzima wa kukuza na kuhakikisha na wanadumu na wachezaji ambao ni matunda ya chuo chao.
 


Tayari wameshapoteza viungo wao wenye vipaji vikubwa, sasa ni Fryers, kinda lingine lenye kipaji aliyekuwa akitaarishwa kuja kuchukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza kumrithi Patrice Evra anaelekea uzeeni - naye yupo njiani kuondoka. Ndio maana wapo tayari kulipa "kodi ya England' kumsanini Leighton Baines.

Lakini hili sio kusema kwamba hakuna wachezaji wengine wakali wanaokuja kutoka kwenye academy, Commitment ya United kwenye kukuza vipaji bado ipo safi kama mawingu. Will Keane amekuwa akifanya mambo makubwa kwenye timu ya reserve na ameichezea England under 21 mwaka huu, ingawa mwezi uliopita alipata majeraha ya goti na atakuwa nje kwa muda kidogo.

Muitaliano aliye na kipaji kikubwa Davide Petrucci ni staa mwingine aliyepo kwenye academy ya United - inaonekana anaweza kuanza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza msimu wa 2012-13 , kinda lenye akili sana kwenye upande wa kushambulia na vision za hatari dimbani - huku beki wa kati Tom Thorpe tayari amecheza kwa kiwango kikubwa mpaka amepewa unahodha wa England under 21.

Pogba, Morrison na Fryers wameondoka, na hili linawapa nafasi United waanze kujifikiria upya. Kuondokewa na wachezaji wake muhimu ni tatizo ambalo limeandama sana Arsenal na limewagharimu sana. United inabidi wajipange na kuweza atleast kuweza kuwalipa vizuri na kuwapa nafasi vijana wao ili wasiendelee kupoteza matunda ya academy yao ambayo kwa hali ya uchumi ilivyo chini ya Glazer - academy ndio nguzo yao kwa sasa.

Vinginevyo wajiandae kuwa chini ya utawala wa mahasimu wao wakubwa wenye misuli ya pesa ambao tayari wamewapora ubingwa wa England msimu uliopita huku wakiwapa kipigo cha aibu.
KWA HISANI YA SHAFFIH DAUDA

No comments:

Post a Comment