skip to main |
skip to sidebar
HATIMAYE FRANCIS CHEKA AFUNGIWA NA TPBO BAADA YA KUGOMA KUPIGANA NA KASEBA
Siku
moja baaada ya kupanda ulingoni na kugoma kupigana na Japhet Kaseba -
taarifa nilizozipata kutoka kwenye chama cha mchezo wa ngumi TPBO ni
kwamba chama hicho kimefungia Francis Cheka kwa kutofanya nae kazi, wala
kutoa kibali chochote cha pambano la aina yoyote limhusulo Cheka.
TAARIFA RASMI KUTOKA TPBO
NDG WAANDISHI WA HABARI [MICHEZO]
AWALI
YA YOTE NINAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU KWA JINSI AMBAVYO
VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKITUSAIDIA SANA KATIKA KUUKUZA
MCHEZO HUU WA NGUMI ZA KULIPWA KWA KUUANDIKA VIZURI SANA NA HATIMAYE
KURUDISHA IMANI KUBWA KWA WAPENZI WAKE AMBAO TAYARI WALIKUWA WAMEUKIMBIA
KUTOKANA NA SABABU AMBAZO MNAZIFAHAMU FIKA ,NA HATA WADHAMINI KUKAA
PEMBENI NA KUUTELEKEZA KABISA.
LAKINI MIAKA ANGALAU MINNE BAADA YA KUPOTEZA MWELEKEO HATIMAYE MASHABIKI WAMEUPOKEA TENA KWA MIKONO MIWILI ,
HIVI
KARIBUNI TAYARI PEPO MBAYA AMEANZA KUJITOKEZA KWA LENGO LA KUUVURUGA
TENA MCHEZO HUU AMBAO NI NGUVU KAZI YA VIJANA KTK KUJIPATIA PESA ZA
KUJIKIMU KIMAISHA KUPITIA NGUMI ZA KULIPWA.
HIVI KARIBUNI VYOMBO
VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKIRIPOT TAARIFA ZA MVUTANO MKUBWA
ULIOJITOKEZA KATI YA BONDIA FRNCIS CHEKA NA WAANDAAJI WA TAMASHA LA
USIKU WA MATUMAINI KUHUSU PAMBANO LAKE NA JAPHET KASEBA HUKU CHEKA
AKIKANUSHA KWAMBA HAKUSAINI MKATABA WA KUCHEZA NA JAPHET KASEBA NA
BADALA YAKE ALISAINISHWA KUPIGANA NA BONDIA KUTOKA MISRI.HAPO TAREHE
07-07-2912 KTK UWANJA WA TAIFA
KIMSINGI TU CHEKA ANAJARIBU
KUWAFANYA VIONGOZI WA KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA -TPBC HAWAJUWI
WAJIBU WAO KWA KUMPA PROMOTA KIBALI CHA KURUHUSU PAMBANO AMBALO NI FEKI
WAKATI SIYO KWELI ,
MIMI BANAFSI NILIPATA NAFASI YA KUONGEA NA
CHEKA NI KWA NINI ALIPIMA UZITO HALI AKIJUA HATACHEZA PAMBANO ? NA KWA
NINI ALIFIKA UWANJANI HALI AKIJUWA HACHEZI PAMBANO ? ALISHINDWA KUNIJIBU
.MAHOJIANO HAYA TULIYAFANYA SIKU YA PAMBANO NDANI YA UWANJA WA TAIFA.
TPBO
INAAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA LENGO LA FRANCIS CHEKA LILIKUWA NI
KUJARIBU KUTENGENEZA MAAFA MAKUBWA AMBAYO YANGESABABISHA UVUNJIFU WA
AMANI KWA KWA MASHABIKI AMBAO WALIKUJA MAHUSUSI KUANGALIA PAMBANO LILE .
NDG
ZANGU WAANDISHI WOTE HEBU JIULIZENI KAMA PAMBANO HILI LINGEKUWA NI LA
KAWAIDA NA LIMEPANGWA KUFANYIKA KATIKA UKUMBI WOWOTE ,NA PROMOTA
AMESHAWATOZA WATU PESA NA WAMEJAA UKUMBINI ,NA KISHA FRANCIS CHEKA
AMEINGIA UKUMBINI NA KISHA KUKATAA KUPIGANA JE MNADHANI MASHABIKI
WANGEKUBALI ? NI LAZIMA WANGEFANYA VURUGU KUBWA AMBAYO INGEWEZA HATA
KUPOTEZA MAISHA YA WATU WENGI SANA NA VYOMBO VYENU VYA HABARI VINGEKUWA
NA KAZI KUBWA SANA YA KUWAHABARISHA WATANZANIA JUU YA MAAFA HAYO AMBAYO
YANGESABABISHWA NA UJINGA WA MTU MMOJA TU FRANCIS CHEKA.
TPBO
IMESIKITISHWA SANA NA TUKIO HILI AMBALO LIMEUVUNJIA KABISA HESHIMA
MCHEZO HUU ,NA HASA UKUZINGATIA KWAMBA VIKUNDI MBALIMBALI VILISHIRIKI
KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI A WASICHANA ,NA HATA WAREMBO WALIJITOLEA
KUPANDA ULINGONI KWA LENGO LA KUCHANGIA ELIMU.
TPBO INAWAPONGEZA
WASANII WOTE WA BONGO MOVIE ,WANAMUZIKI WA AINA ZOTE ,NA WABUNGE WOTE
KWA MOYO WAO WA HURUMA WALIOUNYESHA KUFANIKISHA LENGO LA TAMASHA HILO
.PIA PONGEZI KWA MABONDIA WOTE WALIOKUBALI KUSHIRIKI KUCHANGIA
BONDIA
FRANCIS CHEKA AMESHINDWA KABISA KUWATHAMINI WANAJAMII AMBAO KWA MCHANGO
YAO WAMAWEZA KUMFANYA AJULIKANE TANZANIA NZIMA ,NA AMEWADHARAU SANA NA
AMEUVUNJIA HESHIMA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA KWA UJUMLA WAKE ,NA
AMEUDHALILISHA SANA MCHEZO HUU MBELE YA JAMII YA KITANZANIA NA
AMEWAFANYA MAADUI WASIOUTAKIA MEMA MCHEZO HUU KWA KUTOKUUDHANINI WAAMINI
KWAMBA HUU NI MCHEZO WA WAHUNI NA WAVUTA BANGI .
IMANI ZA TPBO
-------------
KUTOKANA NA MAELEZO YOTE NILIYOYATOWA KWENU NI VIZURI PIA MKAJUWA IMANI ZA TPBO
[1]
TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA INAAMINIWA NA WATANZANIA WOTE WAPENDAO
NGUMI ZA KULIPWA KOTE NCHINI TANZANIA NA INAZINGATIA NIDHAMU NA INAPIGA
VITA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA MICHEZONI ,NA HATA BIASHARA YENYEWE
YA MADAWA HAYO. KWA WANAMICHEZO WOTE NCHINI
[2] TPBO INAAMINI
KABISA KWAMBA NGUMI ZA KULIPWA NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE AMBAZO
HUMPATIA BINADAMU KIPATO CHA HALALI ILI KUJIKIMU KIMAISHA.
[3]TPBO
INAAMINI KABISA KWAMBA HAKUNA BONDIA YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AWEZAYE
KUDHARAU JAMII IILYOMZUNGUUKA NA KUFANYA AWEZE KUFANYA MAMBO AMBAYO
YATAIKERA JAMII HIYO .
[4] TPBO INAAMINI KWAMBA KILA BONDIA ANAZO HAKI SAWA ZA KUTETEWA NA KULINDIWA HAKI ZAKE PAKE ZINAPOKUWA HATARINI KUPOTEA.
[5]
TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAKUZAJI [MAPROMOTA] WATAPEWA MSAADA MKUBWA
PALE WANAPOANDAA MAPAMBANO YAO NA WANAPATA USHIRIKIANO WA DHATI KUTOKA
KWA MABONDIA ,IKWA NI PAMOJA NA KUTANGAZIWA MAPAMBANO YAO KWA
USHIRIKIANO MKUBWA NA MABONDIA WAHUSIKA.
[6] TPBO INAAMINI KABISA
KWAMBA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WANAZO HAKI ZA KUPATA BURUDANI YA
MCHEZO HUU IL WAEENDELEE KUUPENDA KWA FAIDA YA MABONDIA WOTE .
[7]
TPBO INAAMINI KILA BONDIA ANAPASWA KUHESHIMIWA NA HAKUNA BONDIA ALIYE
JUU YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO ZIENDESHAZO NGUMI ZA KULIPWA.
NA
TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA MWENYE MAMLAKA YA KUBADILISHA MPINZANI WA
CHEKA NI PROMOTA NA SIYO BONDIA, NDIPO CHAMA HUSIKA KINATOWA KIBALI KWA
AJILI YA PAMBANO HILO , NA NDIYO MAANA HATA RAIS WA TPBC KUPITIA VYOMBO
VYA HABARI ALIUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KWAMBA ANAITAMBUA MKATABA
/MIKATABA ALIYOISANI FRANCIS CHEKA KUPAMBANA NA JAPHET KASEBA.
MAAMUZI MAGUMU YA TPBO
---------------------------
\
KWA KUWA JAMII YA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WAMEFADHAISHWA SANA NA
TUKIO LILIOFANYWA NA BONDIA FRANCIS CHEKA NAMI NAUNGANA NAO KTK
MFADHAIKO HUO NA KUWAOMBA MSAMAHA KWA TUKIO HILO , NA ILI KUHAKIKISHA
KWAMBA SOTE TUMEFADHAISHWA NA JAMBO HILO-;
TPBO INAMUONDOWA
RASMI BONDIA FRANCIS CHEKA KATIKA ORODHA YA MABONDIA INAOWATAMBUWA NA
HAITAFANYA NAYE KAZI YA IANA YOYOTE KTK ULIMWENGU WA MASUMBWI KTK
KIPNDI CHOTE CHA UHAI WA TPBO. NA UHAI WANGU BINAFI.
HII HAINA
MAANA KWAMBA ANAKATAZWA KUCHEZA NGUMI , LA BALI HUU NI MSIMAMO WA TPBO ,
NA DAIMA MIMI HUIFANANISHA TPBO NA SIMBA DUME LENYE MENO NA AMBALO
HALITAKI KULA MIZOGA , LAKINI KAMA VIKO VYAMA NINAVYODHANI KWAMBA BILA
CHEKA HAVIWEZI KUIMARIKA NA VIMTUMIE SINA PINGAMIZI NAVYO.
TPBO
IPO IMARA NA ITAENDELEA KUWA IMARA KWA KUFANYA KAZI NA MABONDIA WENYE
NIDHAMU NA KATIKA MAAMUZI YETU HATUMUOGOPI YEYOTE ILI MRADI TUMO NDANI
YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO
AHSANTENI SANA
NB- KWA TAARIFA HII NINAUFUNGA RASMI MJADALA KUHUSU BONDI FRANCIS CHEKA.
IMEANDIKWA NAMI ;-
YASSIN ABDALLAH -USTAADH
RAIS-TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION-TPBO
na shaffih
No comments:
Post a Comment