Pages

Monday, July 30, 2012

Hii ndio hali ilivokuwa baada ya Mgomo Wa Walimu Manispaa Ya Singida...!





Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani ktk Manispaa Singida

MGOMO Uliondaliwa na CWT nchini, umeleta madhara katika Manispaa Singida, baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuandamana hadi ofisi ya RC leo.

Kwenye maandamano hayo, watoto wa shule ya msingi Nyerere, Singidani, Ipembe na Unyankindi, walitembea kilomita tatu hadi ofisi ya Mkuu Mkoa, huku barabarani wakiimba ‘tunataka haki zetu, walimu wamegoma, tunataka haki zetu’.

Baada ya askari polisi kubaini usalama wa watoto hao upo hatarini, waliingilia kati na kuongoza maandamano hayo hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wanafunzi hao zaidi ya 600 walijazana katika uwanja wa mbele, jengo la Mkuu wa Mkoa kuanzia saa tatu hadi saa 4:30 asubuhi.

Hatimaye Serikali ya Mkoa kupitia katibu wa tume idara ya Utumishi wa walimu Samweli Ole Saitabau, aliwataka kurudi nyumbani hadi kesho, wakaendelee na masomo katika shule zao

No comments:

Post a Comment