TIMU
ya Yanga leo inakabiliwa na kibarua kigumu cha kutetea ubingwa wake wa
Kombe la Kagame mbele ya Azam katika mechi ya fainali itakayochezwa
uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam leo
Wakati Yanga chini ya Kocha wake Tom Seintfiet ikitaka kushinda kuweka rekodi ya kulitwaa mara ya tano tangu kuanzishwa rasmi michuano hiyo 1974, Azam wanataka kubeba mara ya kwanza.
Wakati Yanga chini ya Kocha wake Tom Seintfiet ikitaka kushinda kuweka rekodi ya kulitwaa mara ya tano tangu kuanzishwa rasmi michuano hiyo 1974, Azam wanataka kubeba mara ya kwanza.
Mbali
ya Yanga kutaka kutwaa taji hilo mara ya tano baada ya kufanya hivyo
mwaka 1975, 1993, 1999 na 2011, Kocha Saintfiet, pia atakuwa akitaka
kuanza vizuri kibarua chake.
Aidha, kama Yanga itafungwa itakuwa imetema taji la michuano hiyo ililolitwaa Julai 10, 2011 chini ya Kocha Mganda, Sam Timbe.
Kikosi cha Yanga leo
Pia,
kufungwa kwake itakuwa pigo kubwa kwa uongozi mpya wa klabu hiyo
ulioingia madarakani Julai 15 kupitia uchaguzi mdogo chini ya Mwenyekiti
wake Yusuf Manji.
Mazingira
hayo, yanaifanya Yanga kucheza kufa na kupona kuhakikisha wanashinda
sio tu kutetea taji, pia kuanza vizuri kwa kocha na uongozi mpya.
No comments:
Post a Comment