Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara
haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza
Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega
Waislamu.
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana
wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara
walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia
fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona…
Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara
haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza
Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega
Waislamu.
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa
Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara
walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia
fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijini.
WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua
jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana hao waliolenga
kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye
Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo
kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya
Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua
mitaa ya Mwenge.
KINONDONI
Baada ya kufagiafagia Sinza kwa
kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni
ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki.
KISA KUHARIBIWA SWAUMU
Kwa mujibu wa vijana
hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa
kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha
kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo
kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00
usiku.
Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari
nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo
akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho
hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha
adabu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari
mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka
kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha
kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”
HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini hao
waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa
Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao
SOURCE GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment