KWA
mtazamo wa kawaida ni kitendo cha kawaida kwa mji wowote kuendelea
kutokana na rasilimali zake zinaouzunguka mji huo. Maeneo mengi nje ya
nchi na hata Tanzania yamekuwa yakipata maendeleo ya jamii na mazingira
yake kutokana na rasilimali na shughuli za kijamii zinazolizunguka eneo
lenyewe.
Hali
hii ni tofauti na ilivyo katika Mji mdogo wa Maganzo uliopo wilayani
Kishapu, Mkoa wa Shinyanga, ambao umefanikiwa kuwa na rasilimali ghali
yenye thamani kubwa ulimwenguni. Mji huu una madini ya almasi
yanayopatikana karibia sehemu kubwa ya eneo la Maganzo.
Kihistoria
Mji wa Maganzo unachimbwa madini ya almasi tangu kitambo kidogo.
Wananchi wanachimba madini hayo katika mashamba, viwanja na maeneo
mengine ambayo yanaaminika kuwa na almasi. Huu ni utajiri mkubwa ambao
Mji mdogo wa Maganzo umefanikiwa kuwa nao.
Baadhi
ya wananchi wamefanikiwa kunufaika na utajiri huu. Nasema hivyo maana
ukifika katika eneo hilo utashuhudia nyumba za thamani na za kisasa na
hata magari ya kifahari ambayo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameyapata
kutokana na almasi.
Mji
huo unahuduma ya umeme, afya (japokuwa kunachangamoto kadhaa),
mawasiliano (mtandao wa simu) na pia umefanikiwa kupitiwa na barabara
kuu ya lami inayotoka Shinyanga mjini kuelekea Mkoa wa Mwanza. Kwa kiasi
fulani mji unavutia.
No comments:
Post a Comment