Pages

Thursday, July 5, 2012

Precision Air yapata Boeing mpya, yafanya safari yake ya kwanza leo



 Ndege mpya ya Precision Air aina ya Boeing 737-300 ikiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere tayari kwa kufanya safari yake ya kwanza kuelekea Lusaka, Zambia kupitia Lubumbashi – Congo DRC mapema leo.
 Taswira ya ndani ya Boeing 737-300 iliyowasili wiki iliyopita toka Nairobi, Kenya ilipokuwa ikibadilishwa muonekano wake kwa kupakwa rangi za Precision Air, pamoja na kuipatia kibali cha kuruka katika anga za Tanzania na kimataifa pia.
Sehemu ya mkia wa ndege hiyo inayo onyesha usajili wake nambari 5H-PKS. Precision Air pia ina ndege Boeing 737-300 mbili zingine zenye usajili 5H-PMS na 5H-PAZ. Kwa ujumla sasa shirika hilo la ndege 12; ATR 72-500 tano, ATR 42 -500 mbili, ATR 42 -320 mbili na B737 -300 tatu.

No comments:

Post a Comment