Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 1, 2012

SIMBA NA EXPRESS HAKUNA MBABE TAIFA



 Mechi kati ya Simba SC na Express imemalizika Uwanja wa Taifa, kwa sare ya bila kufungana. Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha pili. Ilikuwa mechi nzuri.
 Amir Maftah akitibiwa na Dk Cossmas Kapinga baada ya kuumia
 Jingo Suleiman wa Express, anaweza kuwa mchezaji mfupi zaidi Afrika Mashariki na kati kwa sasa
 Kaimu Nahodha wa Simba, Uhuru Suleiman baada ya mechi
BIN ZUBEIRY na Mussa Mudde wa Simba
Mechi ya kirafiki kati ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC na mabingwa wa Uganda inaingia katika kipindi cha pili na timu na hizo hazijafungana. Katika dakika 45 za kwanza, timu zimeshambuliana kwa zamu. Habari njema ni kiungo Patrick Kanu Mbivayanga kutoka DRC, anacheza mpira wa hali ya juu. Katika safu ya ulinzi, Masombo amesimama imara. Simba inacheza soka ya kuvutia kwa kuonana. Imejaza viungo wengi Amri Kiemba, Shomary Kapombe, Mussa Mudde, Mbivayanga na Uhuru Suleiman na wanafanya kazi nzuri. Abdallah Juma, ambaye unaweza kusema Emmanuel Gabriel amerejea Simba anawapa kazi mabeki wa Express, ingawa kipindi cha pili ametolewa. Kipa Albert Mweta amefanya kazi nzuri na anajiamini mno. 
Kikosi kilichoanza Simba SC
Hatari langoni mwa Express
Abdallah Juma kulia akilitia misukosuko lango la Express
Krosi ya Uhuru, jamaa kanawa refa kapeta
Benchi la Simba SC... na bin zubery

No comments:

Post a Comment